Habari za Punde

Kamati ya Kuzuiya Uhalifu Baharini Yakutana Jijini Dodoma.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabilian ana Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akiongoza kikao cha kamati hiyo Mei 30, 2022 katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabilina na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu imekutana na kufanya kikao  cha dharura kwa lengo la kujadili mkataba wa ununuzi wa boti ya doria litakalosaidia kukabiliana na vitendo hivyo nchini.

Kikao hicho kimesimamiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu katika ukumbi wa ofisi hiyo  Mei 30, 2022 jijini Dodoma  kikihusisha Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali na wadau wa maendeleo.

Miongoni wa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Bw. Gabriel Migire, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdallah Kirungu, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw. Sergio Valdini na Mwakilishi wa Balozi wa Japan Tanzania Bw. Tabuchi Tomoyoshi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabilian ana Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw. Sergio Valdini akichangia hoja wakati wa majadiliano katika kikao hicho.
Mtaalamu wa Mradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw.Emmanuel Nnko akiwasilisha taarifa kuhusu hatua za ununuaji wa boti ya doria wakati wa kikao hicho.
Mwakilishi wa Balozi wa Japan Tanzania Bw. Tabuchi Tomoyoshi  (wa kwanza kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu wakifuatilia kikao hicho.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.