Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohammed Said amezindua mradi wa usambazaji vifaa vya kuhifadhia taka uliobuniwa na taasisi isiyo ya kiserikali Kawa Training Centre akisema jukumu la usafi wa fukwe za Mji Mkongwe ni la wananchi wote na si la Serikali pekee.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika zoezi la kuwe usafi wa mazingira katika ufukwe wa pwani ya Forodhani Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kuzindua mradi wa usambazaji vifaa vya kuhifadhia taka uliobuniwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Kawa Training Centre iliyoko Zanzibar.Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika zoezi la kuwe usafi wa mazingira katika ufukwe wa pwani ya Forodhani Unguja Jijini Zanzibar,akiwa na Wadau kutoka Taasisi ya Kawa Training Centre iliyoko Zanzibar.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika zoezi la kuwe usafi wa mazingira katika ufukwe wa pwani ya Forodhani Unguja Jijini Zanzibar,akiwa na Wadau kutoka Taasisi ya Kawa Training Centre iliyoko Zanzibar.Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said amesema kwamba jukumu la kuhakikisha usafi katika fukwe za Mji Mkongwe ni la wananchi wote na sio serikali au taasisi fulani .
Aliyasema hayo wakati akizindua rasmi mradi wa usambazaji wa vifaa vya kuhifadhia taka(Dustbin)uliobuniwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya KAWA Training Centre iliyopo Zanzibar.
Mhe.Simai alisistiza kwamba uwepo wa fukwe ni moja kati ya vivutio vinavyopatikana katika visiwa vya Zanzibar hivyo basi kadiri tunavyoziweka katika hali ya usafi ndivyo idadi kuwa ya watalii itakavyozidi kuongezeka.
Nae mkurugenzi wa Kawa Training Centre Bi Suzanne Degeling ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Waziri kwa kukubali wito wa kushiriki katika kufanya usafi katika fukwe hizo pamoja na kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo. Pia aliwashukuru wadau wote waliofanikisha zoezi hili wakiwemo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kupitia Afisi ya Jiji la Zanzibar, hoteli zote zilizoko katika fukwe za Zanzibar.
Bi Degeling ameeleza kwamba wamekuwa wakifanya usafi katika fukwe za Shangani kwa wiki sita na wanatarajia kuongeza eneo la usafi kuanzia maeneo ya Mizingani hadi kufikia Mazizini katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort na kusisitiza jamii kuwaunga mkono ili kuipendezesha Zanzibar.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Waziri Simai alichangia shilingi Milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mradi huo na kumpongeza kijana kutoka tumbatu Mohammed Jumă Omar kwa jitihada zake za kusafisha fukwe hizo. Kwa kuonesha kufurahia tukio hilo Mhe.Simai alitoa udhamini wa kwenda kisiwa cha Kojani kwa ajili ya uhamasishaji na kutoa elimu ya umuhimu wa kuweka eneo hilo katika hali ya Usafi.
Jana tare 14/05/2022 Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said alijumuika na wakaazi wa Mji Mkongwe pamoja na taasisi zisizo za kiserikali za KAWA na NGOZA katika Usafi wa ufukwe kuanzia skuli ya Tumekuja hadi Forodhani kulikoenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa vyombo vya kuhifadhia taka.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano
Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
15/05/2022.
No comments:
Post a Comment