Habari za Punde

Balozi Mhe.Mulamula Amekutana na Kuzungumza na Jaji wa ICJ

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)  ili iweze kunufaika zaidi na kazi za Mahakama hiyo yenye hadhi ya juu duniani.

Ahadi hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati wa  mazungumzo na Jaji wa Mahakama hiyo, Jaji Abdulqawi Yusuf yaliyofanyika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Aidha, wamejadili ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Taasisi ya Afrika ya Sheria za Kimataifa yenye Ofisi zake Jijini Arusha ambayo Jaji Abduqlqawi ni Mwenyekiti. Taasisi hiyo imejikita kwenye kutoa mafunzo na kufanya tafiti kwenye masuala yanayohusu Sheria za Kimataifa.

Jaji Yusuf alimhakikishia Balozi Mulamula utayari wa Taasisi hiyo kuendelea kutoa mafunzo kwa watanzania kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu Sheria za kimataifa. 

Kwa upande wake Balozi Mulamula alieleza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake kama kupitia Mkataba wa Uenyeji.

Taasisi ya Afrika ya Sheria za Kimataifa ilianzishwa mwaka 2012 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutoa mafunzo na kufanya tafiti kwenye masuala yanayohusu Sheria za kimataifa na Sheria za Umoja wa Afrika na kuvijengea uwezo Vitivo vya Sheria vya Vyuo Vikuu vya Afrika na Wanasheria wa Afrika wanaoshughulika na Sheria za Kimataifa.

Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.