Habari za Punde

DC MOYO Awataka Makarani,Maudhui na Watu wa Tehama Kutanguliza Uzalendo Kutekeleza Zoezi la SENSA

Mwenyekiti wa kamati ya Sensa Wilaya ya Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa ya watu Makazi wilayani humo kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa  zoezi la SENSA la kitaifa
Mwenyekiti wa kamati ya Sensa Wilaya ya Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa ya watu Makazi wilayani humo kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa  zoezi la SENSA la kitaifa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa kamati ya Sensa Wilaya ya Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewataka Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa ya watu Makazi wilayani humo kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa  zoezi la SENSA la kitaifa ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo iliyoyakusudia ya kuwahesabu watu kama ambavyo inatakiwa kuwa Mwaka huu. 


Akizungumza na Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa wanaoendelea na mafunzo katika Manispaa ya Iringa Moyo alisema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi ili kufanikisha zoezi hilo muhumu litakalosaidia upangaji wa bajeti sahihi ili kuiwezesha kufikisha huduma za msingi katika Kila Kona ya nchi hivyo ni muhumu watu waliopewa dhamana ya kutekeleza zoezi hilo wakalitekeleza kikamilifu na kwa weledi wa hali ya juu. 


Moyo aliwataka wahusika wa zoezi la Sensa kuhakikisha wanatunza Siri za taarifa za watu watakaowahesabu  ikiwa ni pamoja na utunzaji wa  vitendea walivyopatiwa na Serikali katika kutekeleza zoezi Hilo. 


Alisema kuwa mhusika yeyeto yule wa zoezi la Sensa atakayepoteva au kuvuruga zoezi la Sensa serikali itamchulia hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi,hivyo kila mhusika anatakiwa kuwa makini na zoezi hilo la kitaifa kwa manufaa ya nchi ya Tanzania.  


Aidha Mohamed Moyo amewaonya Makarani hao pamoja na Watu Wote watakaobainika kuzembea katika utekelezaji wa jukumu walivyopatiwa na Serikali ikiwemo watu Wote wanakajihusisha na uhujumu Kwa lengo la kukwamisha shughuli za Sensa itakayifanyika Rasmi Agosti 23 mwaa huu. 


Akifafanua zaidi amewataka Wananchi kuwa Tayari kwani kuanza   Tarehe 21 Hadi 22 Agosti Mwaka huu Karani wa Sensa akiongozwa na kiongozi wa eneo husika atafika kwenye eneo alilopangiwa kujitambulisha na kutambua mipaka ya eneo lake hivyo Kila Mwananchi awe Tayari kutoa ushirikiano Ili kufanikisha zoezi Hilo. 


Moyo alimazia kwa kuwaomba wananchi wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanahamasishana kujitokeza kuhesabiwa siku ya zoezi la Sensa kwa ajili ya manufaa yao na serikali kujua namna gani ya kupanga bajeti ya eneo husiku kupitia SENSA hiyo ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.