Habari za Punde

Rais Mhe. Samia amuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Majaji wa Mahakama Kuu pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka wakila kiapo cha Maadili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka pamoja na Majaji Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu aliowaapisha Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.