MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka Mabalozi wateule wanaokwenda
kuwakilisha Tanzania nchi za Zimbabwe,
Zambia na Uholanzi kuitumia vyema Diplomasia ya Kiuchumi kwa kuzitafuta na kuzileta Tanzania fursa za kiuchumi
zilizoko kwenye nchi hizo ili ziweze kuisaidia nchi.
Mhe. Othman ameyasema hayo
alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi
Simon Sirro anayekwenda Zambia,
Balozi Luten General Metheu anayekwenda
Zimbawe na Balozi Caroline Chipeta anayekwenda kuwakilisha Tanzania katika nchi
Uholanzi.
Mhe. Makamu amesema kewamba katika
nchi zote hizo wanazokwenda zipo fursa nyingi
za kiuchumi na kiutaalamu ambazo zinaaweza kuisaidia Tanzania
kujiendeleza zaidi kiuchumi iwapo
mabalozi hao watafanya juhudi ya kuzileta nyumbani na kuweza kusaidia nchi yao.
Amewaleza Mabalozi hao kwamba
katika nchi za Tanzania ikwemo Zanzibar
zipo fursa nyingi za kuchumi hasa katika kukuza na kuendeleza sekta ya
utalii , biashara na kilimo maeneo ambayo
hayajatumika ipasavyo na kwamba mabalozi hao ni vyema wakajitahidi
kuifanya kazi ya kuzitangaza ili zitumike kuisaidia nchi.
Amesema nchi ya Zambia inauwezo
nzuri wa kusindika bidhaa za nyama na kwamba utaalamu huo unaweza ukatumika
kuisaidia Tanzania kuongeza thamani ya bidhaa hizo na kuwa na Tija zaidi kwa
nchi kuliko ilivyo sasa.
Aidha amewaeleza mabalozi hao
kwamba Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya maji ya bahari kusogea katika
maeneo ya kilimo na kuathiri ardhi za kilimo na kwamba nchi ya Uholanzi
utaalamu wao unaweza kutumika kuisaidia Zanzibar katika kulikabili vyema tatizo
hilo .
Mhe. Othman amekumbusha mabalozi
hao kuzitumia vyema fursa zinazopatikana katika Mashirika ya Kikanda na
Kimataifa ikiwemo shirika la Kimataifa wabunifu ( WIPO), ili teknlojia na
ubunifu wao uweze kuwasaidia vijana wa Tanzania katika jitihada za kukuza
uchumi na maendeleo yao na Taifa kwa jumla.
Naye Kiongozi wa Mabalozi hao IGP
Mstaafu wa Tanzania Simon Sirro ameeleza kwamba maelekezo wanayoyapata kutoka
kwa viongozi wakuu ni nyenzo muhimu katika kazi yao na kwamba watajitahidi
kuyatumia na kuyafuata katika kutimiza lengo na wajibu waliopewa kuiwakilisha vyama Tanzania kwenye nchi
wanazokwenda.
Amesema kwamba yeye wenzake watajitahidi
kuhakikisha kwamba wanafanya wajibu wao vizuri wa kuitangaza nchi na
kushirikiana na watangulizi wao kupitia Diplomasia ya kiuchumi kukidhi
matarajio ya taifa katika kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment