Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi (kulia) alipofika kutoa pole kwa kufiliwa na Mtoto wake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi, Chukwani Nje ya Jiji la Zanzibar,Mkoa MJini Magharibi (katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Rais) Mbunge wa Fuoni Mhe.Abass Ali Hassan Mwinyi,marehemu Hassan amezikwa Mangapwani Wilaya ya kaskazini “B” Unguja.[Picha na Ikulu] 01/09/2022.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan leo ameifariji na kutoa mkono wa pole familia
ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kutokana na kifo cha
mtoto wake Hassan Ali Hassan kilichotolea juzi usiku katika Hospitali kuu ya
Mnazi mmoja na kuzikwa jana Kijijini kwake Mangapwani Mkoa Kaskazini Unguja.
Hafla hiyo ambayo iliambatana na dua ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Chukwani, Mkoa Mjini Magharibi, ambapo pia Mama Samia alipata fursa ya kutoa mkono wa pole kwa Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi, Mama Siti Mwinyi , Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariam Mwinyi, Mke wa marehemu Fauzia Salim Hilali pamoja na wanafamilia.
Rais Samia alimuomba Mwenyezi Mungu
amsamehe marehemu madhambi yake na kumpumzisha kwa amani, huku akiwataka wafiwa
kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Siti Mwinyi (kulia) Kizuka wa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Bi,Fauzia Salim Hilal (wa pili kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kushoto) wakiitikia dua iliyoombwa nyumbani kwa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar.[Picha na Ikulu]
01/09/2022.
Baadhi ya Wanafamilia na Watoto wa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Mtoto wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi wakiitikia dua iliyoombwa nyumbani kwao Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar,wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipofika kutoa pole kwa msia walioupata. [Picha na Ikulu] 01/09/2022.
No comments:
Post a Comment