Habari za Punde

Waislamu watakiwa kujitathmini ili wafikie malengo


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Al-hajj Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia waumini wa Masjid TAQWA ZIWANI POLISI baada ya Ibada ya Swala ya Ijumaa  Leo tarehe 30/09/2022

Na Ally Mohammed, OMPR

Wazanzibari na waislamu kwa ujumla wametakiwa kujitathmini kwa lengo la kufikia malengo waliojiwekea.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo alipojumuika na Waumini katika Masjid TAQWA ZIWANI POLISI katika swala ya Ijumaa.

 Ameeleza kuwa ni wajibu wa kila Mzanzibar na Muislamu kwa ujumla kujitathmini kwa kila hatua hasa katika masula ya ubadhilifu wa Mali za Umma, Wizi, Madawa ya kulevya, Rushwa pamoja na Udhalilishaji mambo ambayo hurejesha nyuma maendeleo ya wazanzibari.

Mhe. Hemed amesema watu wenye tabia ya kuyafanya matendo haya maovu ni wale wasiofata misingi ya dini hivyo ni vyema kushirikiana kuwapiga vita watu wa aina hii ili kuweza kujiletea maendeleo nchini mwetu.

Alhajj Hemed amewataka waumini na wananchi kwa ujumla kurudi katika misingi ya kidini na kuangalia wapi wamekosea ili kuhakikisha nguvu kazi ya vijana haipotei na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha  inaleta maendeleo kwa wananchi wake wote.

Amesema kila mmoja kwa wakati wake kuhakikisha anasimamia vyema familia yake ili kuondokana na hasara ambayo inaweza kujitokeza kwa vijana wetu.

Alhajj Hemed amesema kuwa Serikali itahakikisha inatimiza wajibu wake kwa wananchi wake wote kwa kuyapiga vita matendo maovu na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali ili kuweza kupata maendeleo hapa nchini.

Kwa upande wake Imamu wa Msikiti huo Shekh. MOH’D RAMADHAN amesema ni wajibu wa kila muumini kuyafanya yale yote ambayo ameyafanya Mtume Muhamad S.A.W hasa katika mwezi huu ambao kazaliwa kipenzi cha waumini wote.

Amesema ni wajibu kwa kila muumini kujifunza na kuimarisha Ibada ili kuweza kupata manufaa hapa duniani na kesho akhera.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.