RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj
Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali,waumuni wa dini ya
kiislamu,familia pamoja na wananchi wa
Jimbo la Dimani katika Dua Maalum (Khitma) ya kumuombea Mwanasiasa Mkongwe wa
Zanzibar Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini aliefariki Alkhamis Usiku wa tarehe
20 Oktoba 2022 Nyumbani kwake na Kuzikwa
kijijini kwao Bweleo,Wilaya ya Magharibi ‘B’,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Hitma hio ya kumuombea Marehemu Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini imefanyika katika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Bweleo ambapo Sheikh Mussa Ali Kirobo ndie alieongoza Dua hio (Hitma)ya kumuombea Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini.
Katibu Mtendaji
wa Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Khalid
Ali Mfaume aliwasihi waumini na wananchi waliojumuika katika Dua hio kuyakumbuka
mema ya Marehemu ambayo aliyokua akiyatekeleza wakati wa Uhai wake huku
akimuelezea kuwa Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame alikua Mtaratibu,Mwenye
kumuheshimu kila mmoja,muungwana na ni mwenye kumsikiliza mtu haja zake. Huku
akiongezea kuwa Mauti inatosha kuwa ni ukumbusho na mawaidha kwa kila mmoja.
Akisisitiza kuwa Dunia sio yetu licha ya kupambwa na kila aina ya Mapambo
mazuri.
Vile vile alimuombea dua Marehemu Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na amjaalie awe miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu.
Mara baada ya kukamilika kwa dua hio Sheikh Ibni Ahmed Haji alitoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kujumuika nao katika kumuombea Mzee wao,huku akisisitiza shukrani za dhati kwa Serikali nzima pamoja na Chama cha Mapinduzi kwa kuwa karibu na familia hio tokea msiba umetokea hadi kufikia siku hio ya Dua maalum na kuchukua nafasi hio kumuombea dua za kheri Rais Dk.Mwinyi katika kuiongoza Zanzibar.
Alhaj Dk.Mwinyi akiwa Msikitini hapo alipata muda wa kuwapa pole familia ya marehemu pamoja na kuwakabidhi Ubani.
Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini katika Uhai wake alishika Nafasi mbalimbali za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Chama cha Mapinduzi ikiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Ikulu,Waziri wa Fedha na Mipango,Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii pamoja na kuwa Mwakilishi wa kuachaguliwa na Wananchi katika Jimbo la Dimani tokea mwaka 2000 hadi 2020 na kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa.
“Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Tutarejea”.
Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha Hitma ikisomwa na Sheikh Mussa Ali Kirobo.(hayupo pichani) kumuombea Marehemu Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini kilichofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Bweleo Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 23-10-2022, na (kulia kwa Rais) Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume na (kushoto kwa Rais) Mwalimu Khamis.
Wanafamilia na Ndugu wa Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini wakiitikia dua ya kumuombea iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Bweleo Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 23-10-2022.
Wananchi wa mbalimbali na wa Kijiji cha Bweleo wakiitikia Dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Bweleo Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 23-10-2022.
Wananchi wa mbalimbali na wa Kijiji cha Bweleo wakiitikia Dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Bweleo Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 23-10-2022.
Mwakilishi wa Familia ya Marehemu Mwinyihaji Makame Mwadini Sheikh.Ibni Ahamad Haji akizungumza na kutowa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Bweleo Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo 23-10-2022.
No comments:
Post a Comment