Habari za Punde

DC Moyo Ameamuru Kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgera

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo  akitoa  onyo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mgera kujisalimisha kwa jeshi la polisi Iringa
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Iringa Mrakibu Mwandamizi Bernad Samara akitoa onyo kwa mwenyekiti wa kijiji cha Mgera kujisalimisha kwa jeshi la polisi Iringa


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ameamuru kukamatwa kwa mwenyekiti wa Kijiji cha Mgera Lucas Mgata kwa tuhuma za kuchochea migogoro ya ardhi kwa wananchi wa Kijiji hicho. 

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alitoa amri ya kusakwa kwa mwenyekiti huyo anayetajwa kukiuka amri ya Serikali iliyositisha kwa muda matumizi ya ardhi katika eneo hilo ili kuchunguza madai ya wananchi kuporwa ardhi na kiongozi huyo. 

Aidha katika mgogoro huo yameibuka matukio yenye kuhatarisha usalama wa wananchi ikiwemo kuchomwa moto uzio wa nyumba zipatazo sita hatua iliyoilazimu Kamati ya ulinzi na usalama kuanzisha kura za siri kumbaini mhusika. 

Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Iringa Mrakibu mwandamizi Bernad Samara alitoa amri ya mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mgera kujisalimi polisi kutokana ukaidi wa amri ya serikali 

Alisema kuwa Mwenyekiti huyo Lukasi mgara analalamikiwa na wananchi wa kijiji cha Mgera kupora maeneo ya wananchi hali iliyoilazimu kamati ya ulinzi na usalama kupiga marufuku ya kufanyika kwa shughuli za kibinaadam katika eneo hilo kupisha uchunguzi wa mgogro huo 

Kufuatia mgogoro huo unaoendelea kwa sasa yameibuka matukio ya kuchomwa moto kwa uzio wa nyumba taklribani sita pamoja na mashamba ya wananchi hatua hii imemlazimu mkuu wa wilaya ya Iringa kufika kijijini hapona kunzisha kura ya siri kumbaini mhalifu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.