Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi aufungua Masjid Hussein Ghana na kujumuika na wananchi katika sala ya Ijumaa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi  alipowasili katika viwanja vya Masjid Hussein Ghana Kichakani Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Msikiti na kujumuika na Wananchi katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo baada ya kuufungua leo 18-11-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la Ufunguzi wa Masjid Hussein Ghana Kichakani Wilaya ya Kati Unguja leo 18-11-2022, na kujumuika na Wananchi wa Ghana katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Hussein Ghana Kichakani Wilaya ya Kati Unguja, na kujumuika na Wananchi wa Kijiji hicho katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo leo 18-11-2022.(Picha na Ikulu)


WANANCHI wa Kijiji cha Ghana Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Hussein, baada ya kuufungua leo 18-11-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Ghana Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Masjid Hussein Ghana Kichakani, baada ya kuufungua leo 18-11-2022.(Picha na Ikulu)  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Hussein Ghana Kichakani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 18-11-2022.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.