Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary
Senyamule akikabidhiwa vyumba 14 vya madarasa na ofisi 9 za
walimu zilizokamilika kwa fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa
vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Hafla hiyo imefanyika
katika Shule ya Sekondari Bahi leo Desemba 12,2022. Wengine katika picha ni
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Bahi Bwana Athumani Masasi
Halmashauri ya Wilaya
ya Bahi ikiwa ni miongoni mwa Halmashauri 8 za mkoa wa Dodoma zilizopewa fedha
za ujenzi wa vyumba vya madarasa ilipokea shilingi Milioni 280 tarehe 8 Oktoba,
2022 na imeweza kuwa Halmashauri ya kwanza kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo
na kukabidhi tarehe 12 Disemba, 2022 huku kila darasa likiwa na viti 40.
Akisoma taarifa
ya ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bwana Athumani Masasi
amesema kuwa ‘’Vyumba vya madarasa 14 na ofisi 9 vimejengwa katika shule zote 8
za Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ikiwemo shule ya sekondari ya Bahi iliyo
kabidhi vyumba 5 na ofisi 2, Idihwa darasa 1 na ofisi 1, Kigwe madarasa 2 na ofisi
1, Chikola darasa1 na ofisi 1, Chipanga darasa 1 na ofisi 1, Chibelela darasa 1
na ofisi 1, Msisi Juu madarasa 2 na ofisi 1 na Lamaiti darasa1 na ofisi 1’’.
Aidha Mhe.
Senyamule ametoa pongezi kwa Halmashauri hiyo na kutaka iwe ya mfano kwa
Halmashauri nyingine zilizopo ndani ya mkoa na kusema;
‘’Mhe Rais wa
Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati ya kutaka kuondoa ujinga kwa
kuimarisha sekta ya Elimu ambapo ametoa fedha za kuongeza vyumba vya madarasa
8,000 nchi nzima ambapo kwa mkoa wa Dodoma tumepata jumla ya vyumba vya
madarasa 339” RC Senyamule
Sambamba na hilo
Mhe. Senyamule ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa kuweza kufanya
vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2022 kwa kuweza kuwa katika
orodha ya Shule 10 bora zilizo fanya vizuri kitaifa ambapo kwa mkoa wa Dodoma
ni Halmashauri hiyo pekee ndiyo iliyoweza kuingia katika 10 bora.
Hata hivyo RC
Senyamule ameongeza kuwa Mhe. Rais ametekeleza miradi ya maendeleo kwa zaidi ya
asilimia 80 kwa Mkoa wa Dodoma huku vituo vya afya, zahanati, madarasa na
huduma zingine zikizidi kuimarishwa.
No comments:
Post a Comment