Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashuhudia Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora - Kigoma (km 506), Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora kwenda Kigoma (km 506) kati ya Serikali kupitia Shirika la Reli (TRC) chini ya Mkurugenzi wake Masanja Kadogosa na Wawakilishi wa Kampuni za ubia za CCECC na CRCC kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC) nchini Masanja Kadogosa na Mwakilishi wa Kampuni za ubia za CCECC na CRCC wakibadilishana Hati mara baada ya kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora kwenda Kigoma (km 506) iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC) nchini Masanja Kadogosa na Mwakilishi wa Kampuni za ubia za CCECC na CRCC wakionesha Hati mara baada ya kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora kwenda Kigoma (km 506) iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora kwenda Kigoma (km 506) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.