Habari za Punde

Utiaji saini ya Makubaliano ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe na bustani ya Forodhani





Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuwajengea Mazingira bora na rafiki Wananchi na Wafanyabiashara mbali mbali Zanzibar ili kuzidi kuinua hali ya Uchumi nchini

Ameeleza hayo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohamed Said alipokua akizungumza na Wananchi waliofika katika hafla ya Utiaji saini ya Makubaliano ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe na bustani ya Forodhani ilofanyika leo katika eneo la bustani ya forodhani kisiwani Unguja.
Akizungumza na Wananchi na wadau mbali mbali waliofika katika hafla hiyo Mhe. Simai amesema “Jitihada zimekua zikifanywa na Serikali ya awamu ya nane katika kuinua Uchumi wa nchi yetu ikiwa pamoja na kuwaekea Mazingira bora Wafanyabiashara mbali mbali ili kujikwamua kiuchumi”.
Aidha Mhe. Simai ametoa onyo kali kwa wale wote wanaojaribu kuzirejesha nyuma juhudi za Serikali kwa kutoa lugha chafu kwa Wateja na Wageni wanaofika katika Eneo hilo, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Nae Afisa Mkuu wa wateja binafsi na biashara wa Benki ya NMB - ndugu Filbert Mponzi amesema kwamba benki yao imekua karibu sana na wananchi na Serikali katika kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ya kuiletea Maendeleo Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.