Habari za Punde

Dk Dimwa akutana na Afisa Itifaki wa Ubalozi wa Marekani nchini

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed(wa kwanza kulia),akizungumza na Afisa Itifaki kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Kristin Mencer (wa kwanza kushoto).

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

 

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed (Dimwa),amesema CCM itaendelea kuthamini na kulinda misingi ya demokrasia kupitia uchaguzi huru na wa haki.

 

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na ujumbe wa Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,ameeleza kuwa uchaguzi huru ndio chimbuko la uwepo wa amani ya kudumu nchini.

 

Dkt.Dimwa, alisema katika Chama Cha Mapinduzi kimejipanga vizuri kuhakikisha Zanzibar inakuwa na amani na utulivu wa kudumu.

 

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa, alisema Zanzibar kwa sasa ipo shwari kutokana na kuwepo kwa amani inayotoa nafasi kwa wananchi kushiriki kwa uhuru katika shughuli za maendeleo.

 

"Zanzibar kwa sasa ipo shwari kila mwananchi ana uhuru wa kufanya kazi halali za kujiingizia kipato kwa muda wowote pia hata hata harakati zingine za kimaisha zikiwemo kufanya ibada na kuabudu.

 

Amani hii haikupatikana kwa miujiza bali ni kwa juhudi kubwa zilizofanywa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Serikali yake inayolinda tunu ya amani na utulivu sambamba na kuimarisha misingi ya demokrasia",alisema DKT.Dimwa.

 

Dkt.Dimwa, alisema CCM inathamini uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani imesaidia kudumisha umoja na mshikamano kwa Wazanzibar wote.

 

Alitamka wazi kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani wameanza kuleta choko choko zinazolenga kuhatarisha maridhiano hayo yaliyopo katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

 

Dkt.Dimwa, alisema  Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 Ibara ya 9(a) imeahidi katika kipindi cha miaka mitano kazi kubwa itakayofanywa na CCM ni kuimarisha maridhiano, kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

 

Aliwambia wawakilishi hao wa Marekani kuwa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi, amekuwa akitekeleza Ilani ya CCM kwa kasi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya afya,elimu,kilimo,uwekezaji,usafiri wa baharini na nchi kavu,diploma na maji safi na salama.


Pamoja na hayo,aliishauri mwakilishi huyo kutoa fursa za udhamini wa masomo hasa katika fani za Sayansi,biashara,Uchumi na Siasa.

 

Alisema kupitia dhana ya uchumi wa blue wananchi wengi wananufaika na uvuvi wa bahari kuu kwani kampuni kubwa zikivua samaki hao wanaonufaika ni wananchi wa chini.

 

Alieleza kwamba Serikali imeendelea kutafuta njia mbadala ya kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira kwa kuwawezesha wananchi mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na benki za umma. 

 

Naye Afisa Itifaki kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Kristin Mencer,alisema lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha pamoja na kuendelea mahusiano ya kiutendaji.

 

Alisema Marekani inahamasisha demokrasia katika nchi mbalimba Duniani ili Wananchi waishi kwa amani.

 

Alieza kuwa Marekani imekuwa ikitoa fursa mbalimbali za udhamini wa masomo kwa vijana wa Zanzibar ili wawe na uwezo kukabili soko la ajira Kimataifa.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.