Mstahiki Meya wa jiji la Zanzibar
Mahmoud M, Mussa amewasisitiza vijana kuwa wazalendo na kuwacha
kujishirikisha na vitendo viovu vikiwemo vya udhalilishaji na matumizi ya
dawa za kulevya ili taifa lipate viongozi bora.
Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi
vijana yalioyoandaliwa na Raha Tv Online Mahmoud amesema viongozi vijana
wanamchango mkubwa katika kuchochea maendeleo kwa taifa lao hivyo si vyema
kutumika katika vitendo viovu ambavyo vinarejesha nyuma maendeleo ya
taifa na hatimae kushiriki kikamilifu katika kuinua uchumi wa nchi.
Awali akimkaribisha mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Suzan Peter Kunambi amewataka.vijana
kutokata tamaa katika kuzisimamia ndoto zao ili zikamilike sambamba
na kuutaka uongozi wa Raha Tv Online kuwa wabunifu ili jamii ifaidike na
habari mbali mbali ikiwemo za kuelimisha na kuburudisha .
Katibu Mtendaji Tume ya
Utangazaji Zanzibar Suleiman Abdullah amesema Tume kwa kushirikiana
na TCRA zitaendelea kuvisimamia vyombo vya habari nchini ili kuona
vinafuata utaratibu na maadili ya utangazaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Raha Tv Online ndugu
Raya Hamad Mchere amesema Raha Tv Online inalengo la kuwapasha habari vijana na
wanawake na jamii kwa ujumla kuhusu mambo mbali mbali ikiwemo kuhabarisha,
kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha
Mafunzo hayo yaliyobeba ujumbe ‘MIMI
NI WA THAMANI’ yana lengo la kuwajengea uwezo Viongozi vijana na kuwawezesha
kujua thamani yao na umuhimu wao kwa nchi, kwa vile wana wajibu wa kuhakikisha
kuwa wanathamini jitahada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwainua kiuchumi na hatimae malengo yao
kufanikiwa.
Mafunzo hayo yamewashirikisha viongozi vijana kutoka Baraza la
Vijana Zanzibar, Vyuo Vikuu viliopo Zanzibar na wengine kutoka taasisi zisizo
za kiserikali ambapo Mkurugenzi huyo amaesema mafunzo elekezi yatakuwa chachu
ya kufahamu kwa kina changamoto za vijana na njia za kuwajengea uwezo ili wawe
vijana wazalendo na kufuata sheria za nchi hii bila kushurutishwa.
Mafunzo hayo yamefungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Ndg Muhammed Ali Abdalla ‘teacher Muha’ ambapo ameupongeza uongozi wa Raha Tv
Online kwa kuwa na malengo mazuri ya kuwajengea misingi imara kwa kuamsha ari
na kujenga uwelewa wa masuala ya kiuchumi kijamii pamoja na masuala mtambuka
katika kuleta chachu na kuwainua kitaaluma katika kuwainua Viongozi vijana hatimae
kuwa tayari na wajibikaji
Ameuomba uongozi wa Raha Tv Online kutoishia bali mafunzo hayo yawe
ni endelevu na kuwataka viongozi vijana kuwa wana jukumu kubwa na kuonesha
mabadiliko katika jamii na kuonesha uzalendo wenu kwa vitendo kubadilisha akili
za baadhi ya watu kwa kutambua Zanzibar ni moja kuikomboa kiuchumi ilipo na
kuipeleka kwenye maendeleo zaidi ambayo Serikali yetu inakwendanayo
Amesema Raha Tv Online iwe ni chemchem ya kuwajengea uwezo vijana ili
waondokane na utegemezi wawe wabunifu katika utayarishaji kwa uwezo waliokuwa
nao kuendeleza vipaji vyao katika kuyasarifu mazingira tuliyonayo na fursa
zilizopo.
Mada kadhaa ziliwasiliwa zikiwemo Uzalendo iliyowasilishwa na Bw
Mwalimu Ali Mwalimu Katibu Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
kujitambua na uongozi, Itifaki ndg Mussa Yussuf, uongozi na matumizi ya vyombo
vya habari Dkt Mnemo mhadhir chuo cha Habari.
Mada nyengine zilihisu udhalilishaji na maadili Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana Taifa ndg Yunus Ali Juma, UKIMWI Mkurugenzi Tume ya UKIMWI Dkt
Ahmeid M. Khatib, ushuhuda na historia ya maisha Dkt Rukaiya Wakif Kamishna
Idara ya Mipango Zanzibar, mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika kwenye ukumbi wa chuo cha
Zanzibar School of Health kilichopo Kwa Mchina mwanzo.
No comments:
Post a Comment