Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipojumuika na waumini wa masjid Nurullah Magomeni Wilaya ya Mjini katika Ibada ya sala ya ijumaa.
Alhajj Hemed ameeleza kuwa Azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuijenga Zanzibar yenye Maendeleo na kuwataka Wananchi kuwa Mstari wa mbele katika kuhakikisha Zanzibar inafikia maendeleo hayo.
Ameeleza kuwa tayari miradui mbali mbali ya mendeleo imeanza kuzinduliwa na mengine inaendelea kwa hatua mbali mbali ya kukamilika ambapo kutazalikafursa za ajira kwa vijana wenye fani mbali mbali ili kupunguza changamoto ya ajira Nchini.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaeleza waumini hao kuishauri serikali kwa mambo mazuri na kukemea tabia ya baadhi kubeza yanayofanywa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kuhusu suala la utunzaji wa Amani ambayo ndio kinga ya nchi yetu Alhaji Hemed amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuilinda hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha matendo maovu ikiwemo udhalilishaji na madawa ya kulenya ambayo yamekuwa ni majanga makubwa nchini.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema jamii ya sasa ni ya kutegemeana hivyo ni Vyema kuwasaidia wanaohitaji jambo ambalo litaongeza umoja, Mshikamano na Upendo katika Jamii.
Akitoa Khutba katika Sala hiyo Shekh Abdallah Hassan Ali amewakumbusha Waumini hao kutumia vyema mwezi huu Mtukufu wa Shaaban kwa kufanya matendo mema kama alivyokuwa Kiongozi wa umma huu Mtume Muhammad (S.A.W).
Amesema miongoni mwa sifa za Waumini ni kujipamba na tabia njema pamoja na kujikita katika Ibada hasa kuomba msamaha kwa Mola Mtukufu kwa yote waliyokosea.
No comments:
Post a Comment