MAKAMU wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , amejumuika na Viongozi,
wafuasi wa na Wanachama wa Chama cha
Act- Wazalendo pamoja na waumini wa Dini
katika haluli ya kumuombea Dua aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.
Dua hiyo
iliyofanyika katika Masjid Omar Bin khattab katika mtaa wa Msubiji ni kumbukumbu
ya kutimia miaka miwili tangu kufariki kwa kiongozi huyo mashuhuri mnamo tarehe 17 Februari mwaka
2021.
Marehemu
Malim Seif alifariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa kwa
matibabu kwa kipindi cha takribani wiki mbali baada ya afya yake kodorora zaidi
alipokuwa amelezwa awali kwa matibabu katika Hospitali ya Mnanzi mmoja.
Akitoa
wasifu wa Kiongozi huyo baada ya kukamilika kwa dua hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu
ya ACT- Wazalendo Nd. Hassan Jani Masoud, amesema kwamba kiongozi huyo alikuwa
na mwenendo bora na kuwa msamehefu kwa kila aliyemkosa.
Amesema kwamba
maalim Seif aliwajali wanancho wote na hasa wanyonge na hakuwa mkachu wa tabia
sambamba na kujitoa katika kutetea maslahi ya Zanzibar na watu wake bila
kuchoka katika maisha yake yote.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu amewataka wananchi
wa Zanzibar kuishi na sifa ya maalim Seif kwa kuwa alikuwa ni mtu mstahamilivu,
msamehevu na aliyejiweka katika dara la kati aliyeishi vyema na watu wa aina
zote hata wale waliomkosa.
Aidha
amesema kwamba maalimu seif alikuwa kiongozi
mwenye huruma aliefuata vigezo na maelekezo mema katika kusimamia na
kuwaongoza wananchi na wafuasi wake jambo lilomfanya kupata mapenzi kwa watuwatu
wengi ndani na nje ya Zanzibar.
Naye Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Nd. Salim Biman kwa niaba ya Viongozi
wawakuu wa Chama hicho amesema kwamba anawashukuru watu wote waliokusanyika
katika maeneo mbali nchini kumuombea dua marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.
Dua kama
hiyo imesomwa katika misikiti mbali mbali ya Unguja na Pemba , Dar es
Salama na kwengineko kwa nia ya
kumkumbuka na kumuombea kwa mwenyezimungu amsamhe makossa yake na amuweke
mahali pema Peponi.
Mwisho.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari
leo tarehe 17.02.2023.
No comments:
Post a Comment