Habari za Punde

Mkurugenzi Mamlaka ya mji mkongwe awataka wananchi kufuata utaratibu

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Ali Saidi Bakari akikemea na kutoa taarifa ya uchimbaji mashimo bila kibali wakati akizungumza na waandishi Habari huko Ngome kongwe Zanzibar tarehe 3/02/2023. 

Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale, Mariam Mohamed Mansab akitoa maelezo kuhusiana na mabaki ya binaadamu kwa waandishi wa Habari huko Ngome Kongwe Zanzibar tarehe 3/02/2023.

fisa wa Mambo ya Kale Faki Othman Haji anaeshughulikia tafiti mbalimbali akieleza kuhusu chungu kilichofinyangwa kwa jiwe kwa wandishi wa habari kilichokutwa katika shimo huko Ngome Kongwe 3/02/2023 . 

 Vifaa mbali mbali vilivyokutwa kwenye shimo ikiwemo mabaki ya mifupa ya  binaadamu  huko Ngome Kongwe 3/02/2023.
 Vifaa mbali mbali vilivyokutwa kwenye shimo ikiwemo  vigae vya sahani, meno na chungu kilichofinywanga kwa jiwe huko Ngome Kongwe 3/02/2023.

Na Khadija Khamis – Maelezo, 03/02/2023 .

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Ali Said  Bakari ametoa wito kwa wananchi wanapotaka kuchimba katika maeneo ya mji mkongwe wafuate utaratibu wa kupatiwa kibali .

Akiyasema hayo huko Mji Mkongwe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  uchimbaji wa shimo la maji taka ambalo lilikutwa na mabaki ya mifupa ya binadamu pamoja na magae  ya vitu mbali mbali vya thamani.

Amesema kupewa ridhaa na mamlaka yeyote kufanya kitu chochote cha maendeleo katika mji  mkongwe bila kupatiwa kibali ni kosa kisheria

Nae Mkurungezi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Mariam Mohamed Mansab amesema shughuli zozote zinazohusiana na uchimbaji kwa Zanzibar ni vyema kuhusishwa na Idara ya Mambo ya Kale  

Aidha alifahamisha kuwa jambo hilo kutokezea bila ya  kupatiwa taarifa mapema imeharibu  utafiti ambao ungesaidia historia ya Zanzibar .

“ Wananchi mngelitoa taarifa mapema kwa mamlaka ya mji mkongwe kungesaidia kufanyika utafiti kujuwa sehemu hiyo ilikuwa ya kitu gani.”alisema Mkurungezi huyo.

Nae Afisa wa  Mambo ya kale Faki Othman Haji amesema katika shughuli mbalimbali za utafiti alizofanya hajawahi kuona chungu kilichofinyangwa kwa jiwe na kuwekwa marembo pamoja na  kupata vitu hivyo vitasaidia historia ya Zanzibar  .

Alifahamisha kuwa wananchi wanahitaji kupatiwa elimu ili kufahamu taratibu zilizopo katika mji mkongwe iwapo watafanya shughuli zozote za kimaendeleo ikiwemo ushimbaji kuwasiliana na mamlaka husika .

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.