Habari za Punde

Tanzania kuanza safari za moja kwa moja Saudi Arabia

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Abdulwahab wakikabidhiana zawadi baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini akijadiliana jambo na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Abdulwahab katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Tanzania inategemea kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah inatarajiwa kuanza tarehe 26 Machi 2023.

 

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo ya Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab na kujadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia.

 

Katika mazungumzo yao viongozi hao pia walijadili mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.