Habari za Punde

Mkurugenzi TAMWA-ZNZ Ataka Asasi Za Kirai Zijitathmini

Asasi za kiraia Zanzibar (CSOs) zimetakiwa kujiwekea utaratibu maalumu wa kujipima kila baada ya kipindi cha miezi miatatu kwa lengo la kujitathmini na kuambua njia bora za kufikia malengo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa wakati alipokua akizungumza na baadhi ya wawakishi wa asasi 30 kutoka Unguja na Pemba katika mkutano uliofanyika kwenye umbi wa Chama hicho Tunguu wilaya ya kati Unguja.

Alisema Asasi za kiraia zina mchango mkubwa wakuleta mabadiliko kwenye jamii, hivyo wana wajibu wa kujiewekea utaratibu maalumu ambao utawapa fursa wahusika kujitathmini na kujua wapi walipo na wanataka kufanya nini.

Alisema ili Asasi hizo ziweze kuendelea kufanya kazi zao kwa maslahi ya jamii wanapaswa kuacha kufanya kazi kwa mazoea wakiamini kuwa kila kitu ni rahisi na wataweza tu kutimiza wajibu wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji mwevuli wa Asasi za kirai Zanzibar (ANGOZA) Mwalim Hassan Khamis Juma alisema mkutano huo ni muhimu sana katika kupata taarifa za awali zinazohusiana na maswala ya utetezi ambazo, zitapelekea kujua mapungufu yaliopo hatimae kuchukuliwa hatua za kujengeana uwezo ili kukabiliana na mapungufu hayo.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo kujikita zaidi katika mambo muhimu ambayo yataorodheshwa na kisha kujadiliana kwa pamoja ili walio mwengi zaidi waweze kufaidika.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo Maulid Sleiman kutoka (ZYF) alisema mkutano huo ni muhimu sana kwa maslahi ya Asasi na jamii kwa ujumla.

Alisema kukutanishwa pamoja kwa Asasi kunatengeza mahusiano mazuri sambamba na kujifunza kile ambacho wengine wanatekeleza na kuamini kuwa ni jambo muhimu sana.

Nae Zawadi Abdalla Khamis kutoka taasisi ya (ZGC) alisema mkutano huo utatoa mwanga na kutambua madhaifu yao kama wawakishi wa taasisi zao na ndio njia kuu itakayopelekea mabadiliko.

Mkutano huo wa siku moja umeitishwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na shirika la Foundation for Civil Society.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.