Na.Mwandishi wa OMWKR.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amewataka wananchi kuendelea kushikamana
na mafunzo yanayopatikana katika mwezi
mtukufu wa ramadhani kwa kufanyanyiana ihsani kwa wenye uwezo kuwasaidia
wenye kipato duni.
Mhe. Othman ametoa kauli hiyo, huko
Mombasa Wilaya yas Magharib B alipokuwa akitoa majumbuisho ya zaira yake ya
kuwatembelea wangonwa na wenye misiba kama ni ada inayofanywa kila mwaka ikiwa
ni muendelezo wa mtangulizi wake marehemu
Maalim Seif Sharif Hamad.
Mhe. Othman ambaye pia ni Mkamu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo amefahamisha kwamba ramadhani inatoa
mafunzo makubwa kwa waumini kuweza kushiakamana
na kuendeleza mambo ya kheir na kwamba kusaidiana ni moja wapo ya mafunzo
muhimu yanayopatikana katika mwezi mtukufuu wa mfungo wa Ramadhan.
Mhe. Makamu amesema kwamba pia
waumini watumie mafunzo ya mwenzi mtukufu wa ramadhani kwa kusamehe na kusamehena
katika masuala mbali mbali ya makossa yualiyotokea aili kwa pamoja ziweze
kupatikana kheri za mola mumba.
Mhe. Othman amewataka wagonjwa
kuendelea kuwa na subra licha ya mtiani wa maradhi yaliyowapata na kuwataka
kufahamu kwamba maradhi ni mtihani kutoka kwa mola muumba kumkumbuka mja wake
na kuwaombea kwa mwenyezimungu wapone haraka ili waweze kushiriki katika
shughuli zao za kujitafutia riziki na ujenzi wa taifa.
Amefahamisha kwamba kuwatembelea
wagonjwa kunajenga imani kwa anayetembelewa lakini pia ni ada inayotokana na
dini na kwamba waezee wamefuata miongozo
hiyo hivyo ni vyema kwa pamoja kuiendeleza.
Mapema Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Mkoa Magharib ‘B’ Kichama
Ndugu Ali Juma amesema kwamba ziara hizo zinasaidia sana katika kujenga hamasa
kwa jamii katika kuona kwamba viongozi wanashirikiana na kushikana vyema na
wanaowaongoza katika jamii.
Mhe. Othman amemaliza ziara yake ya
kuwatembelea wagonjwa na wenye misiba katika mikoa yote ya Unguja ambapo leo
amemalizia katika majimbo ya wilaya ya Magharib ‘A’ na ‘B’ Unguja na na
anatarajiwa kufanya ziara kama hiyo
kisiwani Pemba mapema wiki ijayo.
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake cha habari leo tarehe 29.03.2023.u
No comments:
Post a Comment