Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Yatoa Tamko Kuelekea Siku ya Kifua Kikuu Duniani

Naibu Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Fatma Kabole Akizungumza wakati alipokuwa Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari  kuelekea siku ya Kifua kikuu Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo machi 24, kauli mbiu ya mwaka huu "ndio tunaweza kumaliza kifua kikuu" hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar
Meneja wa Kitengo Shirikishi Ukimwi ,Homa ya Ini na Ukoma Mohammed Jabir Dahoma akijibu baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano na   Waandishi hao kuelekea  siku ya Kifua kikuu Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo machi 24, kauli mbiu ya mwaka huu "Ndio Tunaweza Kumaliza Kifua Kikuu" hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar 
Naibu Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Fatma Kabole Akizungumza wakati alipokuwa Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari  kuelekea siku ya Kifua kikuu Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo machi 24, kauli mbiu ya mwaka huu "ndio tunaweza kumaliza kifua kikuu" hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar

Na Fauzia Mussa,Maelezo                                   

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kitengo Shirikishi cha Ukimwi ,Homa ya Ini na Ukoma  imedhamiria kuongeza mapambano ili  kufikia malengo ya   kuutokomeza Ugonjwa wa  Kifua Kikuu ifikapo 2030

 

Naibu Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Fatma Kabole ameyasema hayo  huko  Wizara ya Afya Zanzibar wakati alipokua Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuelekea siku ya Kifua kikuu Duniani .

 

Amesema katika kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya mwaka huu  Wizara ya Afya imeandaa mikakati madhubuti ya kupambana na janga hilo kwa  Kuongeza Mashine za kisasa zenye uwezo mkubwa zaidi wa kupima Sampuli za wenye dalili za Ugonjwa huo.

 

Aidha alisema Wizara imejipanga kununua Gari maalum yenye vifaa vya uchunguzi ambayo itafika katika Shehia mbalimbali  kupima wanananchi wenye dalili za ugonjwa huo ili kuwatambua mapema na kuepusha kuongezeka kwa maambukizi mapya .

 

Akielezea Takwimu za Shirika la Afya Duniani  za mwaka 2021 Naibu Fatma alisema kwa upande wa Zanzibar  jumla ya wagonjwa 1077 waliripotiwa wana ugonjwa huo   kwa 2022 ukilinganisha na wagonjwa 1090 waliogunduliwaa mwaka 2021, kumi na tano kati yao  waligundulika kuwa na kifua sugu .

 

Alifahamisha  kuwa Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu si jukumu la Wizara ya Afya Pekee hivyo kunahitajika nguvu za pamoja katika kutokomeza ugonjwa huo ili kuiokoa jamii kwani wastani wa watu thelethini kufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo .

 

Naibu huyo alisema  kuwa bado jamii ina uelewa mdogo juu ya dalili za ugonjwa huo hivyo wananchi hushindwa kufika Vituo vya Afya jambo linalopelekea   kutofikia idadi ya  Wagonjwa waliotarajiwa kugundulika kila mwaka.  

 

“kuna wimbi kubwa la watu wenye dalili za ugonjwa huu katika jamii na bado  hawajafika katika vituo vya afya kwa uchunguzi  hivyo nawaomba Wanachi kufika katika vituo vya Afya mara waonapo dalili za Ugonjwa huo ikiwemo kukohoa kwa wiki mbili au zaidi na kupata makohozi ya damu,”Alishauri Naibu huyo.

 

Nae Meneja wa Kitengo Shirikishi Ukimwi Homa ya Ini na Ukoma Mohammed Jabir Dahoma amesema  kundi la Wanaume Kati ya miaka 25 Hadi 55 wapo hatarini zaidi kuathirika na ugonjwa huo kutokana na harakati zao za kazi na mfumo wa maisha .

 

Maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu Duniani huadhimishwa kila ifikapo Machi 24 ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu ni “NDIO TUNAWEZA KUMALIZA KIFUA KIKUU”

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.