Habari za Punde

Siku ya Kinamama Mama ni Nguzi Muhimu katika Maendeleo ya Nchi

Siku ya Akina mama Duniani Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma amezungumza na akina mama mbalimbali wa watoto yatima kwa lengo la kuwanasihi namna ya kuwalea vizuri na watoto hao.

Akiwa katika Skuli ya Maandalizi na Msingi Sebleni Mjini Unguja Mhe Riziki amewaomba kina mama hao kuhakikisha wanawafuatilia watoto wao kwa ukaribu zaidi ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji.

Amesema mama ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Nchi,  hivyo ni vyema kuwa mstari wa mbele katika kuwalea vizuri watoto wao ili kupata Taifa bora la baadae.

Aidha amweaomba akina mama kuendelea kumuombea dua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ili azidi kuleta maendeleo nchini pamoja na kuiombea dua nchi ibaki kuwa na amani na utulivu.

Nao akina mama wamesema watajitahidi kushirikiana katika malezi kwa watoto wao ili kuwalinda na vitendo vya Udhalilishaji.

Hata hivyo wameelezea kufurahishwa juu ya kasi ya  Rais Dkt Huessein Ali Mwinyi katika kuiletea Maendeleo Zanzibar na kiahidi kumuombea dua na kumuunga Mkono ili kuleta maendeleo zaidi nchini.

Mhe Riziki amezungumza na akina mama wanaoishi na watoto yatima baada ya kufika katika Skuli ya Msingi Sebleni kwa lengo la kupatiwa kupokea msaada nguo, sare za skuli pamoja na   vifaa mbalimbali vya kusomea vivyotolewa na Jumuiya ya Assalaam kwa kushirikiana na Jumuiya ya Stichting Goodness Will Save The World kutoka Holland na Uturuki.

Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano, Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.