Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Acti Wazalendo Zanzibar
Mhe. Othman Masoud Othman aewataka wanachama wa
chama hicho kuendelea kushirikiana katika kuunga mkono juhudi za pamoja za ujenzi wa
matawi ya chama katika majimbo mbali mbali ili kuwa na ofisi rasmi za chama
hicho.
Mhe. Othman ameyasema hayo kwa nyakati tofauti huko
katika Kijiji cha Koani Kibonde Maji Jimbo la Tunguu na Ndijani Kiunga Ndege Jimbo la Chwaka wilaya ya Kati Unguja
aliposalimia wanananchi na wanachama wa chama hicho baada ya kuweka mawe ya
msingi ya ujenzi wa matawi kwenye maeneo hayo.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar amesema kwamba chama ni taasisi muhimu
na kwamba juhudi za kuwepo ujenzi wa ofisini ni alama za chama katika
kuendeleza juhudi za pamoja za kuimarisha taasisi na kuwa na mahala bora pa
kufanyia kazi.
Amewataka wa wanachama wa chaka hiyo kuendelea
kushirikiana na kujitolea kwa hali na mali katika kuunga mkono juhudi za ujenzi
wa ofisi za Chama zinazoanzishwa katika
maeneo na majimbo mbali mbali.
Ametoa wito kwa
wananchama na wapenzi wa chama hicho kuendelea kujitolea katika
kuimarisha uhai wa chama kwa kuendeleza ujenzi wa matawi mbali mbali na kwamba
juhudi hizo zinaendelea kuungwa mkono na viongozi katika ngazi tofauti ili
kuweza kufanikisha maelengo ya chama.
Mhe. Othman amefahamisha wanachama hao kwamba juhudi
za pamoja ndio njia ya pekee itakayosaidia chama hicho kufikia malengo yake ya
kuhakikisha kwamba wanasaidiana kwa pamoja katika kuleta maslahi bora ya
Zanzibar ili kuweza kufikia lengo la kupatikana maendeleo ya Zanzibar.
Amewataka wanachama wa chama hicho kuendelea
kushajiishana na kushikamana katika kuunga mkono juhudi mbali mbali
zinazoanzishwa na wanachama na viongozi katika ngazi tofauti kwa maendeleo ya
Zanzibar.
Naye Mwanasheria Mkuu wa ACT – Wazalendo ambaye pia ni
waziri wa Biashar na Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban amesema kwamba ni muhimu kwa viongozi na wanachama
kushirikiana katika kuendeleza jitihada za pamoja na kuimarisha chama.
Amesema kwamba viongozi mbali mbali wapo tayari kujitolea kwa hali na mali kuungana na juhudi
za wanachama katika kutekeleza jitihada za pamoja za kuleta maendeleo ya chama
ikiwemo ujenzi wa ofisi za matawi na
majimbo ili kuleta uhai wa chama hicho.
Mhe. Othman yupo katika katika muendeleo wa ziara za kuetembelea mjaimbo mbali mbali katika mkoa wa kusini iliwa ni muendelezo wa kuhutubia mkitano ya hahdara katika majimbo mbali mbali Unguja na Pemba na baadae atahutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho huko chwaka wilaya ya Kati Unguja.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar
30, Julai, 2023
No comments:
Post a Comment