Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Elimu Zanzibar Nd. Abdallah Mohammed Mussa amewataka kisiwani Pemba kuwasimamia walimu waliopata mafunzo ya utekelezaji wa mtaala mpya ili waweze kuwaandaa wanafunzi kiumahiri.
Ameyasema hayo katika kikao maalumu cha majadililiano kilichowashirikisha Maafisa hao huko katika ukumbi wa Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo Amali Chake Chake Pemba.
Aidha Nd. Abdallah amesema kua nilazima Walimu wawe na Makubaliano katika ufundishaji nakusisitiza kwamba Mtaala wenyewe hauna tatizo lolote bali nijukumu la Walimu kuufanyia kazi kulingana na mafunzo waliyopatiwa.
Nae Mkurugenzi Idara ya Maandalizi na Msingi Bi Fatma Mode Ramadhani ameelezea matumaini yake juu ya kufanikiwa kwa malengo ya mtaala huo licha ya changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika hatua za awali za utekelezaji wake.
Amesema ili Mtaala uitwe mtaala hauna budi kupitia hatua mbali mbali na kupata Baraka za watu tofauti hivyo anaimani kwamba mtaala huo upo salama na utatoa matokeo bora kama ulivyokusudiwa.
Amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu inafanya jitihada za kutatua changamoto mbalimbali za zinazowakabili Walimu katika Utekelezaji wa Mtaala huo.
Wakitoa hoja mbalimbali katika kikao hicho Maafisa wa Elimu wamesema idadi kubwa ya wanafunzi madarasani, utungaji wa mitihani uliojikita katika muundo wa mtaala mkongwe na Walimu kukosa uwiano katika ufundishaji ni baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa mtaala mpya.
No comments:
Post a Comment