Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi azungumza na ujumbe wa wachezaji wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Ikulu

WACHEZAJI wa Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakiwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-7-2023, kwa ajili ya mazungumzo,  na kutembelea  sehemu za Historia ya Zanzibar katika ziara yao ya siku moja ya Kitalii Zanzibar, wakiwa wageni wa Timu ya Yanga African Sport Club.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI na Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-7-2023 kwa mazungumzo na kutembelea sehemu za Utalii Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Rais wa Timu ya Yanga African Sport Club Mhandisi Hersi Said akizungumza na kuitambulisha Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kuitambulisha Timu hiyo baada ya kumaliza mchezo wao wa Kirafiki wa Tamasha la Wananchi lililofanyika tarehe  22-7-2023 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Da es Salaam. Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo kwa bao 1-0.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya Jezi ya Yanga ikiwa na Jina lake na Rais wa Timu ya Yanga Mhandisi Hersi Said, baada ya kumaliza mazungumzo na Ujumbe wa Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs  wakiongozana na Viongozi wa Yanga, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-7-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakiongozana na wenyeji wao Timu ya Yanga African Sports Club, kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, wakiwa Zanzibar kwa ziara ya siku moja kutembelea maeneo ya Historia ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu ya Yanga, Kaizer Chiefs na Wachezaji wa Timu hiyo baada ya kumaliza mazungumzo yake na Ujumbe huo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-7-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Viongozi wa Timu ya Yanga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,baada ya kumaliza mazungumzo yake na Ujumbe huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-7-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Viongozi wa Timu ya Yanga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,baada ya kumaliza mazungumzo yake na Ujumbe huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-7-2023 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.