MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama cha ACT –Wazalendo Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman,
amesema kwamba Zanzibar inahitaji kuingia katika Mageuzi yakayofanywa kwa kuzingatia Amani ili nchi iendelee kuendeshwa
kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi
wenyewe wanavyotaka.
Mhe. Othman
ambaye Pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo huko
Chumbuni Wilaya ya Mjini Unguja alipozungunza katika Mkutano wa hadhara wa
chama hicho akiwa katika mfululizo wa mikutano mbali mbali yenye dhamira ya
kuelezea ahadi ya chama hicho kwa wananchi.
Amefahamisha
kwamba hatua hiyo ni muhimu kwani
itasaidia nchi iendeshwe kwa
mujibu wa maono viongozi wa chama na wananchi
wanavyotaka wenyewe ikiwa ni pamoja na kuzingatia haki ya
kuchagua kiongozi na pia kuwa na uwezo wa kuwawajibisha na chama kiendelee kazi
ya kuichunga na kuisimamia serikali.
Amesema
kwamba hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuendelea na kupiga hatua iwapo
wananchi hawana uwezo na mamlaka ya kuwachagua na kuwawajibisha viongozi
wao waliowachagua wanaoshindwa
kuwajibika kulingana na mwatakwa ya wananchi kwa mujibu utaratibu .
Ni busara
viongozi wa serikali kuwa na utaratibu wa kujisema wenyewe jambo litakalosaidia kuwepo utamaduni wa utakaojengwa ndani ya
chama kutimiza ahadi walizoziweka kwa wananchi kwa kuichunga serikali.
Amesema
kwamba ni jambo muhimu kuwepo kwa muungano wenye kuzingatia haki katika mashirikiano ya kusimamia masuala mbali mbali yanayofanywa
ikiwa ni pamoja na kuwepo uwezo wa kupanga kodi kwa mujibu wa hali ya uchumi wa
Zanzibar bila kuwepo vizuizi ama vikwazo vinavyotokana na mashirikiano ya
muungano uliopo.
Akizungunzia Rasilimali ya mafuta na gesi asilia
amesema kwamba chini ya mfumo wa muungano uliopo Zanzibar haina mamlaka ya kisheria kuweza kuchimba mafuta kwa kuwa sharia inayosimamia
rasilimali hiyo ndivyo inavyoeleza hadi sasa.
Amefahamisha
kwamba ni vyema rasilimali ya gesi asilia na mafuta zikazingatiwa kama
rasilimali za dhahabu ni mali ya upande
ilipo badala ya zile zilioko Tanzania
Bara kuwa hazihusiki na Zanzibar lakini ya mafuta na gesi iliytopo Zanzibar
kufanywa kwamba ni ya muungano.
Amewataka
wananchi kuendelea kushirikiana na kushikamana kwa kukiunga mkono chama hicho
kwa kuwa kina maono ya kutafuta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Zanzibar .
Aidha
amewataka wananchi wote ambao hawana Kitambulisho cha Manzibari mkaazi
kuhakikisha kwamba wanafanya juhudi za kujiandikisha ili waweze kupata haki yao
hiyo muhimu ambayo inaambatana na suala la kuwa mpiga kura.
Naye Naibu
Katibu Mkuu wa Chama hicho Nassor Ahmed Mazuri amesema kwamba wananchi
wanapaswa kushirikiana kukiunga mkono chama hicho kuendelea kuwa chama imara
ambacho kimejidhatiti katika kuleta
mageuzi yatakayaosaidia kuondoa matatizo mbali mbali ya umasikini na ya
kijamii.
Kitengo cha
habari
Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
23, Julai,
2023.
No comments:
Post a Comment