Habari za Punde

Mkasaba atoa neno kwa wadau wa kilimo (NaneNane)

Wananchi mbalimbali wakitembelea na kupata elimu kuhusiana na mazao ya kilimo  katika mabanda ya maonesho ya kilimo  yaliyofanyika Dole Wilaya ya Magharibi A.
Zubeda Salim Abdalla kutoka jku akiwapatia wananchi elimu ya utengenezaji na matumizi ya gesi asilia ambayo hutengenezwa kwa kutumia kinyesi cha Ng'ombe katika maponesho ya kilimo yaliyofanyika Dole Wilaya ya Magharibi A
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe  Rajab Mkasaba akipata maelezo kuhusiana gesi asilia ambayo hutengenezwa kwa kutumia kinyesi cha Ng'ombe  kutoka kwa Luteni Kanali wa JKU Ramadhan Ali Hassan alipotembelea  maonesho ya  wakulima yaliyofanyikaWilaya ya Magharibi A

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe  Rajab Mkasaba akipata maelezo kuhusiana na NTA kutoka kwa mfugaji Nyuki wakati alipotembelea maonesho ya ya kilimo yaliyofanyika Dole Wilaya ya Magharibi A

PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANIZIBAR


Na Fauzia Mussa

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe.Rajab Mkasaba amewataka wadau wa kilimo kutumia vyema fursa ya elimu walioipata katika maonesho ya wakulima (nane name) ili kuleta mageuzi ya kilimo Nchini.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho hayo yaliyofungwa Agosti 10 huko Dole Wilaya ya Magharibi A amesema maonesho hayo hayakuwa  kwa ajili ya kujionea bidhaa za kilimo tu,Bali pia yalijikita katika kuwapatia wananchi elimu kuhusiana na kilimo.Hivyo aliwataka wadau hao  kufuata malekezo ya wataalamu ili kuhakiksha wanalima ,kufuga na kufanya shughuli za Uvuvi wa kisasa.

Aidha Mhe. Mkasaba alipongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya kilimo kwa kuboresha maonesho hayo yanayotoa fursa Kwa wakulima ,wajasiriamali na wadau wa kilomo kuweza kutoa elimu kwa wananchi kuhusuiana na  mambo mbalimbali ya Kada hiyo.

Vile vile aliwashauri wadau hao kuwa Mabalozi wazuri kwa wenzao kwa  kuweza kuwapatia elimu,uzowefu na ujuzi walioupata katika maonesho hayo ili kurithisha kilimo bora kizazi hadi kizazi

“kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa wataalamu wametuelekeza kulima kisayansi ,shamba dogo mazao mengi na yenye  bora ni wakati wakubadilika sasa ”alisisistiza Mkuu huyo

Awali  Mkuu wa Wilaya alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuzindua maonesho hayo mwanzoni mwa mwezi huu sambamba na kukubali ombi la Wizara ya kilimo la uboreshaji wa miundombinu ya Barabara katika eneo Hilo Jambo ambalo litawarahisishia wananchi  kufika katika maonesho hayo kwa urahisi.

 Hata hivyo Mkuu huyo alitumia Fursa hiyo kuishauri Wizara ya Utalii na Mambo yakale kwa  kushirikana na Wizara ya kilimo kuhakikisha wanayatangaza zaidi maonesho hayo kwa  wageni wanaotoka Nchi mbali mbali kuja Kutalii Zanzibar  katika Msimu wa Maonesho ili wawe daraja la kuitangaza Zanzibar kupitia  bidhaa adimu zinazotokana na  kilimo Visiwani humu.

"Zanibar tuna matunda adim ambayo  wenzetu hawana kama shoki shoki doriani nashauri  tuwashajihishe watalii kuja kujionea bidhaa hizo ili  na wao waweze kuzitangaza nchi kwao"

Baadhi ya wadau wa kilomo waliojitokeza katika maonesho hayo walisema maonesha yamewasaidia kupata elimu na kubadilishana uzowefu Kati ya wajasiriamali,wakulima,wafigaji na wavuvi

Hivyo wameahidi kuifanyia kazi elimu hiyo na uzowefu walioupata katika maonesho hayo ili kuleta mabadiliko ya kilimo nchini.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wakulima Duniani hufanyika kila ifikapo agosti 8 ya kila mwaka ambapo kitaifa maadhimisho hayo yalifanyika Jijini Mbeya yakiwa na  kauli mbiu “VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA KWA MIFUGO ENDELEVU YA CHAKULA”

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.