Habari za Punde

Nchi 16 za SADC Zashiriki Mkutano wa 43 Luanda Angola

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akishiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Luanda Nchini Angola, ambapi Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo, walioko nyuma ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Jamal Kassim Ali (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk (wa pili kushoto), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Balozi Kennedy Gaston (kushoto), baada ya Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Luanda, Angola.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.