Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Wahandisi Wanawake Tanzania

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano la Wahandisi Wanawake Tanzania linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 3-8-2023.
WASAHIRIKI wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulifungua Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 3-8-2023.
WAGENI Waalikwa katika ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulifungua Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 3-8-2023.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalum na Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania Mhandisi Rehana Juma na (kushoto kwake) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi,wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 3-8-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti Maalumu Mchangiaji Mkubwa wa Kongamano la 8 la  Wahandisi Wanawake Tanzania Kampuni ya Anglogold Ashanti Geita Gold Mining Ltd Makamu wa Rais wa Kampuni ya Anglo Gold Ashanti Afrika Ndg.Simon Shayo, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano hilo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 3-8-2023 na (kushoto kwake) Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania Mhandisi Rehana Juma na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar Mhe.Dkt.Khalib Salum Mohammed wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo leo 3-8-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) wakimsikiliza Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Dar es Salaam  Mariam Ngwali  akitowa maelezo ya ubunifu wa Mashine ya kuondoa mazao shambani na mashine ya kutengeneza juisi, wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2023, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Rehana Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) wakimsikiliza Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Loyola Dar es Salaam Lisa-doris Andrew, akitowa maelezo ya ubunifu wa mashine ya kugundua ufujaji katika matumizi majumbani,wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2023, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Rehana Juma.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) wakimsikiliza Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Lumumba Mariyam Seif,  akitowa maelezo ya ubunifu wa jengo la Skuli ya Lumumba wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2023, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Rehana Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) wakimsikiliza Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kisutu Dar es Salaam Shamsa Jamal Nassor wa Kidatu cha Sita, akitowa maelezo ya ubunifu wa Roboti (Farm Bot) kwa ajili ya kuvunia mazao shambani,wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2023, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Rehana Juma.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) wakimsikiliza Mfanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mine Janeth William Luponelo akitowa maelezo ya uchimbaji wa Dhahabu katika mgodi, wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2023, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 8 la Wahandisi Wanawake Tanzania na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Rehana Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.