Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimuongoza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Hamza Hassan Juma kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Mtumba
Jijini Dodoma muda mfupi baada ya kutembelea eneo la
mradi wa ujenzi wa Majengo ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika
Eneo la Mahoma Makulu, Mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti, 2023.
Wajumbe
wa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ wa Baraza la Wawakilishi
wakipokelewa na wenyeji wao Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe.
Khamis Hamza Khamis mara baada ya kuwasili wakati wa ziara yao ya kutembelea
Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma jana
Jumatatu (Agosti 21, 2023)
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
katikati akiteta jambo na Mkurugenzi Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Bw. Khalid Bakar Amran wakati wa ziara ya
wajumbe wa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ wa Baraza la
Wawakilishi waliotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Majengo ya Taasisi za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Eneo la Mahoma Makulu, Mkoani Dodoma jana
Jumatatu (Agosti 21, 2023).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Hamza Hassan Juma (kushoto) akizungumza jambo wakati wa ziara ya ya wajumbe
wa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ wa Baraza la
Wawakilishi waliotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Majengo ya Taasisi za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Eneo la Mahoma Makulu, Mkoani Dodoma jana
Jumatatu (Agosti 21, 2023). Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais, Mhe. Dkt. Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Viongozi na Watendaji
wa Ofisi hiyo na Wajumbe wa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za
SMZ wa Baraza la Wawakilishi waliotembelea Ofisi hiyo tarehe 21 Agosti, 2023.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akizungumza jambo na Wajumbe wa Wajumbe wa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na
Idara Maalum za SMZ wa Baraza la Wawakilishi mara baada ya kumalizika kwa kikao
baina yao katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe
21 Agosti 2023.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Hamza Hassan Juma (kushoto) wakati wa kikao na wa Wajumbe wa Kamati ya
Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ wa Baraza la Wawakilishi mara baada
ya kumalizika kwa kikao baina yao katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mji wa
Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 21 Agosti 2023.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Hamza Hassan Juma (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya
Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ wa Baraza la Wawakilishi mara baada
ya kumalizika kwa kikao baina yao katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mji wa
Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 21 Agosti, 2023.
(PICHA
NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment