RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ukiongozwa na Kamishna wa TIRA Dr. Baghayo Saqware (kushoto kwa Rais) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 4-9-2023 na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi pia ni Balozi wa Bima Mhandisi Zena Ahmed Said na Mbunge wa Bunge la Tanzania pia ni Balozi wa Bima Mhe. Wanu Hafidh Ameir.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kuanzisha mpango wa kupunguza kiwango kikubwa cha fedha zinazotumika nje ya nchi na badala yake zitumike ndani ya nchi.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu,
Zanzibar alimpozungumza na uongozi wa mamkala hiyo iliyofika kwa lengo la
kuwatambulisha mabalozi wapya wa kuitangaza taasisi hiyo kwenye ngazi ya
viongozi wa kuu wa Serikali za SMZ na SMT, Mashirika ya Umma na taasisi
nyengine za Serikali juu ya umuhimu wa kuendelea kuitangaza kwa umma.
Dk. Mwinyi alisema kwa miaka mingi Serikali
ilikuwa ikikata bima nje ya nchi sasa TIRA imeleta mafaniko makubwa kwa kuokowa
fedha nyingi.
Aidha,
Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza mabalozi wapya walioteuliwa na TIRA kuendelea
kuitangaza taasisi hiyo kwa viongozi wa umma wa Serikali za Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu
wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Ahmeid Saidi, Mhe. Wanu Hafidh Ameir na
Mhe. Japhet N. Hasunga wote ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Naye,
Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware kwenye mazungumzo hayo alimueleza Rais
Dk. Mwinyi mafaniko yaliyopatikana na TIRA kwenye Sekta ya Bima ikiwemo ongezeko
la asilimia 1.68% kwenye pato la Taifa kwa mwaka 2021 kutoka asilimia 0.56% kwa
mwaka 2020.
Pia
alieleza taasisi hiyo imeendelea kuongeza gawio kwa Serikali kutoka mwezi Julai
2022 hadi Juni 2023 kwa kulipa gawio la Tsh. Bilioni 2.9.
Akizungumzia
mafanikio kwenye sekta ya ajira, Kamishna Saqware alimueleza Rais Dk. Mwinyi
kwamba hadi Septemba 2022 TIRA ilitoa ajira za kudumu kwa Watanzania 4, 173
ikilinganishwa na 3,208 kipindi kama hicho mwaka 2021.
Mabalozi
hao wa TIRA, waliteuliwa mwezi Februari mwaka huu, wakikabidhiwa majukumu ya
kutoa ushauri kwa Mamlaka na sekta ya bima kwa ujumla kuhusu maendeleo ya sekta
hiyo pia kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya bima katika ngazi mbalimbali
ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi,
Makatibu Wakuu wa SMT na SMZ, Mashirika ya Umma na taasisi nyengine.
Tangu
kuteuliwa kwa mabalozi hao, tayari wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu
umuhimu wa bima, kutoa elimu kwa umma wakiwemo viongozi wa Umma, wabunge,
wawakilishi, makatibu wakuu, mashirika ya umma na viongozi wa taasisi nyengine
kwa kuwa mstari wa mbele kuishauri Serikali kuhusu umuhimu wa ukataji bima wa
mali za Serikali.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU,
ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment