Habari za Punde

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi yaweka maboya maeneo tengefu


Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kupitia Idara ya Uhifadhi wa bahari imefanikiwa kuweka maboya ya kufungia boti katika maeneo tengefu matatu kwenye Hifadhi ya Bahari ya TUMCA (Mwana wa Mwana) na Hifadhi ya Bahari ya MIMCA (Oba Oba, Dongwe Mlango na Kisiwa cha Mnemba).

Maboya haya yanakwenda kutatua changamoto ya utupaji nanga kwenye matumbawe unaofanywa na maboti yanayopeleka watalii katika maeneo Tengefu kwenye hifadhi zetu.

Hatua hii itasaidia kuhifadhi rasilimali ya matumbawe ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya Uvuvi na Utalii ambazo ndio sekta muhimu za uchumi wa Buluu.

Wizara imelenga kuweka maboya mengine ya kufungia boti katika maeneo mengine katika mwaka huu wa fedha.

Maeneo hayo tengefu ni Mashariki ya Kisiwa cha Bawe, Fungu la Mchanga la Pange/Nakupenda, Kisiwa cha Kwale na Fungu la Mchanga (Safari Blue), na Mwamba wa Hanga, Nungwi.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.