Habari za Punde

Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira yazinduliwa rasmi Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais  Mhe.Harusi  Said  Suleiman  akizungumza machache wakati akizindua Bodi ya Maamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) huko Ofisi za Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais  Mhe.Harusi  Said  Suleiman  akimkabidhi kabrasha lenye nyenzo  za kufanyia kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Maamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Asha Ali Khatib mara baada ya kuizundua bodi hiyo huko Ofisi za Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

Na Fauzia Mussa,      Maelezo

Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira wametakiwa  kufanya kazi kwa uadilifu,weledi, umakini na kujituma ili kuirudisha Zanzibar katika hali yake nzuri ya kimazingira. 

 

Akitoa nasaha kwa wajumbe hao wakati akizinduzi  Bodi hiyo huko Ofisi ya ZEMA Maruhubi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Harusi Said Suleiman   amesema kufanya hivyo kutapelekea dhamira  ya kuteuliwa kwao  kufanikiwa  kwa ufanisi mkubwa.

 

Alisema kwa sasa Zanzibar inakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kulikosababishwa na uchimbaji wa mchanga sehemu zisizo rasmi  pamoja na ukataji wa miti ovyo hivyo bodi hiyo ina kazi kubwa  ya kutatua changamoto za athari hizo   amabazo zimejitokeza nchini.

 

Alisema uwepo wa mazingira rafiki kwa viumbe wa misitu na bahari kunaleta ustawi wa maendeleo ya nchi hivyo aliwataka wajumbe wa bodi hiyo kuzingatia miongozo, kanuni na sheria za kusimamia mazingira ili  kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi juu ya viumbe hao.

 

Waziri Harusi aliwasisitiza wajumbe hao kubuni mikakati ya kidigitali na vyanzo vya mapato ili kuiwezesha Taasisi hiyo kujitegemea na  kuwataka watendaji hao kuwa na mashirikiano mazuri  na Wananchi  ili kugundua kwa haraka athari za kimazingira na kuzipatia ufumbuzi.

Nae  Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa mazingira ZEMA Asha Ali Khatib    amesema bodi hiyo itahakikisha kuwa inatekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuimarisha ustawi wa  mazingira Nchini.

Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira imeteuliwa hivi karibuni kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya  mwaka 2015 ikiwa na  jukumu la kusimamia uhifadhi wa mazingira nNchini

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.