Habari za Punde

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi afanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Colombo, Sri Lanka


 Mheshimiwa Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame jana pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa IORA, unaofanyika Colombo, Sri Lanka,  alikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea Bwana Chung Byun-Won, na kuzungumzia maeneo mbali mbali ya mashirikiano baina ya Tanzania na Korea ikiwemo masuala ya kibiashara, miundombinu, uwekezaji, uchumi wa buluu,  maendeleo ya kijamii, miradi mbali mbali ya maendeleo inayofanyika Tanzania kupitia Serikali ya Korea, pamoja na Mkutano ujao wa Korea na Afrika unaotarajiwa kufanyika mwakani na fursa zinazokuja za mahusiano ya karibu zaidi yanayozidi kukua baina ya Tanzania na Korea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.