Habari za Punde

Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZSHF) Yatoa Mafunzo kwa Wanachama Wake Juu ya Sheria ya Mfuko Huo

Mkurugenzi masoko na uhusiano Mfuko wa huduma za Afya ZHSF Asha Kassim biwi akizungumza na watendaji wa Wizara ya Uchumi wa BulUu na Uvuvi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya mfuko hu,huko maruhubi Mjini Unguja

Mkurugenzi masoko na uhusiano Mfuko wa huduma za Afya ZHSF Asha Kassim biwi akizungumza na watendaji wa Wizara ya Uchumi wa BulUu na Uvuvi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya mfuko hu,huko maruhubi Mjini Unguja.
Ofisa Idara ya uvuvi Ali Khamis  Shadhil  akiuliza maswali kwa maofisa wa mfuko wa huduma za   Afya wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya mfuko huo

Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya Sheria ya Mfuko wa Huduma za Afya.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MALEZO ZANZIBAR

Na Fauzia Mussa ,       Maelezo

Wanachama wa Mfuko wa huduma za Afya  wametakiwa kufuata sheria na miongozo ya ZHSF ili kuzifanya huduma hizo  kuwa endelevu.

 

Akizungumza na watendaji  wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya  Mfuko huo     Afisa Masoko na Uhuinano, Asha Kassim Biwi alisema  mfuko huo umeanzishwa chini ya sheria namba 1 ya mwaka  2023  kwa lengo la  kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu , pamoja  na upatikanaji wa rasilimali fedha   kwaajili ya kugharamia huduma  hizo.

 

Aidha alisema kwa mujibu wa Sheria hiyo  mfuko  una Jukumu la kukusanya ,kuhifadhi na kusimamia  fedha hizo ili kulipia gharama za matibabu kwa Wanachama na Wategemezi wao.

Alifahamisha kuwa Mfuko huo  haukuwalenga watendaji wa Serikali tu kwani sheria ya mfuko imewagawa wanachama  kwa makundi kulingana na kipato cha mwanachama husika.

 

Akizungumzia kuhusu makosa na adhabu katika sheria hiyo amesema sheria inaelekeza kutolewa adhabu kwa mwanachama atakaekwenda kinyume na sheria za mfuko au kufanya uhujumu ikiwemo faini, kifungo au vyote kwa pamoja,hivyo  aliwataka  Wanchama hao kutumia kadi zao pale tu inapohotajika ili kuepusha usumbufu usio wa lazima.

Amesema kila mmoja ana jukumu la kuulinda mfuko huo, pamoja na kuchangia afya ili kuimarisha  na kurahisisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu Nchini.

“Utakapoimarisha Afya ya Taifa umeimarisha Uchumi, bila ya Afya hakuna maendeleo hakuna wafanyakazi, wavuvi, wakulima kwa hali hii uchumi utadumaa” Alifahamisha Mkuu huyo.

 

Nao washiriki wa mafunzo hayo  wameishukuru ZHSF kwa kuwafikia na kuwapatia  elimu inayoenda kuharakisha utendajikazi wa mfuko huo.

 

Walisema tayari ZHSF imeshatoa orodha ya Hospitali zinazotoa huduma hizo  na  taratibu zake hivyo wapo tayari kufuata utaratibu huo  ili kuepusha changamoto zisizo za lazima.

 

Sheria ya mfuko wa huduma za Afya ZHSF ilipitishwa Barazani febuari 28 2023 na kutiwa saini na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi Machi  20,2023 na kuchapishwa  rasmi katika gazeti la Serikali Machi 30 mwaka huohuo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.