Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Akabidhi TUZO Kwa Waazilishi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akimkabidhi Tunzo ya Heshima Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt.Amani Abeid Karume(katikati) akiwa miongoni mwa waanzilishi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  katika Sherehe za Mahfali ya 19 ya Chuo hicho leo katika Kampasi ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohamed Mussa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akimkabidhi Tunzo ya Heshima Ndg.Amour Salmin (katikati)kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt.Salmin Amour akiwa miongoni mwa waanzilishi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  katika Sherehe za Mahfali ya 19 ya Chuo hicho leo katika Kampasi ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohamed Mussa 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akimkabidhi Tunzo ya Heshima Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman akiwa miongoni mwa waanzilishi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  katika Sherehe za Mahfali ya 19 ya Chuo hicho leo katika Kampasi ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohamed Mussa na (kushoto) Makamo Mkuu wa Chuo Prof.Makame Haji. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akipokea Tunzo ya Heshima,kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohamed Mussa ,kwa kutambua mchango wake mkubwa akiwa Mkuu wa Chuo wa kwanza kuanzisha Mkusanyiko wa Kitaalam "CONVOCATION"wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA)  katika Sherehe za Mahfali ya 19 ya Chuo hicho leo katika Kampasi ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.