Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Amefungua Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini "B" Pangatupu

 

Muonekano wa Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini "B"-Pangatupu iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar, ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameifungua leo Januari 11, 2024.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini "B"-Pangatupu iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar, Januari 11, 2024. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nasser Ahmed Mazrui. Uzinduzi wa Hospital hiyo ni sememu ya shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini "B"-Pangatupu iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar, Januari 11, 2024. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nasser Ahmed Mazrui. Uzinduzi wa Hospital hiyo ni sehemu ya shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Zuhura Juma Makame ambaye ni Mhudumu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini "B"-Pangatupu kuhusu mashine ya kusaidia watu wenye matatizo ya moyo. Wakati wa ufunguzi wa hospital hiyo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.