Habari za Punde

Zanzibar Tayari kwa Duru ya Kwanza ya Utoaji wa Vitalu vya Uchimbaji na Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia

Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuivi Mhe. Shaaban Ali Othman akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na uzinduzi wa duru ya kwanza ya utoaji wa  vitalu vya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia unaotarajiwa kufanyika   machi 20 mwaka huu katika Hoteli ya golden tulip,hafla iliyofanyika Ofisi za Wizara hiyo Maisara Mjini Unguja

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya uzinduzi wa duru ya kwanza ya utoaji wa  vitalu vya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia iliyotolewa na Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuivi Mhe. Shaaban Ali Othman (hayumo pichani) huko Ofisi za Wizara hiyo Maisara Mjini Unguja, uzinduzi huo  unaotarajiwa kufanyika   machi 20 mwaka huu katika Hoteli ya golden tulip.

PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR.

Na Fauzia Mussa , maelezo Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa  kuzindua duru ya kwanza ya utoaji wa  vitalu vya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ili kufungua  fursa kwa wawekezaji zitakazoimarisha uchumi wa Nchi.


Akitoa  taarifa kwa umma Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuivi Mhe. Shaaban Ali Othman ameseama uzinduzi huo utafanyika machi 20 mwaka huu katika Hoteli ya Golden tulip uwanja wa ndege Zanzibar .


Aidha amefahamisha kuwa maandalizi yote husika yanayohitajika ili Zanzibar kuweza kutoa vitalu vya wawekezaji kwaajili ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia yamekamilika .

 

“kwa sasa Zanzibar ipo tayari kwa duru ya kwanza ya utoaji wa vitalu katika maeneo ya baharini kwa wawekezaji wa mafuta na gesi duniani kote, jambo ambalo litaiweka zanzibar katika ramani ya dunia kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia.” Alisema Mhe Shaaban

 

Hata hivyo ameziomba   kampuni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia duniani kote kushiriki katika duru ya kwanza ya utoaji wa vitalu vya mafuta na gesi asilia katika maeneo ya baharini na kusema kuwa Zanizbar ipo tayari kupokea na kushirikiana na wawekezaji wote  katika kuendeleza sekta ya mafuta na gesi asilia nchini.

Mapema  alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha suala hilo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Itakumbukwa kuwa Juni 31, 2023 wizara hiyo ilikutana na waandishi wa habari kwa lengo la kuwaeleza wananchi kuhusu kutangaza rasmi ufunguzi wa maeneo mepya ya baharini kwaajili ya utafutaji na  uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa Zanzibar, ambapo wizara ilisema kazi ya kuzichakata data kutoka serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania za ugawaji wa vitalu vipya maeneo ya  bahari iliyopo mashariki mwa Zanzibar imekamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.