Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wanavyuoni na Masheikh Katika Hauli na Dua ya Kumuombea Marehemu Alhabyb Ahmad Bin Abuubkar Sumeit Iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa Malindi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea marehemu Mwanachuoni Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit ikisomwa na Sayy Mudh-hiridin Ally Qullatein (kushoto kwa Rais)  wakiwa katika kaburi la marehemu lililoko katika eneo la  Msikiti wa Ijumaa Malindi Wilaya Mjini Unguja, wakati wa hafla ya Hauli ya 102 iliyofanyika leo 22-4-2024 na (kushoto kwake) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Masheikh na Wananchi mbalimbali katika Kisomo cha Hauli ya 102 ya kumuombe Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit, iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Sheikh. Sayy Mudh-hiridin Ally Qullatein


SAYY.Omar Bin Ally Qullatein akihitimisha kisomo cha Hauli ya 102 ya kumuombea Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit, iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, na (kushoto kwake) Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Masheikh, Wanavyuoni na Wananchi baada ya kumalizika kwa Hauli ya 102 na dua ya kumuombea Marehemu Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit,iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasilimia Masheikh na Wananchi baada ya kumalizika kwa Kisomo cha hitma na dua (hauli ya 102 tangu kufariki kwake) ya kumuombea Mwanachuoni Mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit,iliyofanyika leo 22-4-2024 katika msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Masheikh na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Mwanachuoni marehemu Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit,ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) baada ya kumalizika kwa kisomo hicho kilichofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 22-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Sheikh. Ali Hemed Jabir (Aliyani) baada ya kumalizika kwa Hauli ya 102 na dua ya kumuombea Mwanachuoni marehemu Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit,iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 22-4-2024
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.