MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) John Chikomo, akizungumza na viongozi wa eneo la Makuyuni Wildlife Park, wakati wa ziara ya waandishi wa habari JET, walipotembelea eneo hilo na kuona uhalisiwa wa wanyamapori, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili unaotekelezwa na JET.
(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, ARUSHA)
Na. Abdi Suleiman - ARUSHA.
AFISA Utalii Makuyuni Wildlife Park Chacha
Maramba Masase, amesema kuwa eneo la Makuyuni
Wildlife Park ni lango kuu la utalii Arusha, kwa
watalii wanaokwenda hifadhi mbali mbali kuangalia
Wanyama.
Alisema eneo la Makuyuni lipo kilomita 115 kutoka uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kilomita 71 kutoka jiji
la Arusha, ikizingatiwa eneo hilo lipo katika barabara kuu ya Arusha kwenda hifadhi mbali mbali.
Akizungumza na waandishi wa habari za mazingira Tanzania
(JET), walipofika kujionea mazingira ya eneo hilo, ikiwa ni
utekelezaji wa mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili
unaotekelezwa na JET.
Alisema eneo hilo lipo katika lengo la taifa la kuongeza idadi
ya watalii Tanzania, pamoja na kuongeza wageni wanaotembelea na tokea Oktoba 2023 hadi sasa watalii 239 wametembelea eneo hilo, 52 ni watalii kutoka mataifa ya nje na 187 ni watalii wa ndani.
Alifahamisha kwamba katika muda mfupi huo, tayari
wamekusanya shilingi za Kitanzania Milioni 11,675,000/=,
kutoka kwa wageni wanaotembelea eneo hilo ikizingatiwa
hata msimu wa utalii haujaanza.
“Msimu wa utalii ukifia tunatarajia kuwapokea watalii wengi,
winge waliofika wamevutiwa na uoto wa asili uliopo,
Wanyama wengi wanaonekana kwa urahisi kama vile Twiga, Tembo, Pofu, Nyati, pamoja na kupanda mlima kipara kuona uchomojazi na utuaji wa jua,”alisema.
Nae Afisa Uhifadhi na meneja wa Makuyuni Wildlife Park
uwamangi Andrew Kishe, alisema katika eneo hilo limejaliwa
kuwa na vivutio mbali mbali vya utalii, mandhari yenye
kupendeza, sehemu tambarare, maeneo ya miinuko ya
milima, huku watalii wengi wakivutiwa na kupanda mlima kipara.
Alisema eneo hilo limejaliwa kuwa na kivutio cha
Wanyamapori aina ya kipekee akiwemo Choroa,
ikilinganishwa na maeneo mengine ya hifadhi kama vile
Tarangire, Serengeti, sambamba muonekano wa wanyama
kwa uzuri, Tembo, Twiga, Makundi makubwa ya Pofu, Nyati na Pundamilia.
Akizungumzia suala la ujangili wa wanyamapori, meneja uyo,
alisema TAWA imeweka rasilimali watu na vitendea kazi
katika eneo hilo, kwa kufanya doria za mara kwa mara kwa
kuzunguka ndani na nje ya mipaka ya eneo kuhakikisha
majangili hawapati fursa ya kuua wanyamapori.
“Pia tumezuia uingizaji wa mifugo ndani ya eneo hili, imekua
ni changamoto kubwa kwa jamii iliotuzunguka jamii ya
Kimasai, kipindi cha kiangazi maeneo yao ya nje
wanayotegemea kulisha mifugo yao yakikauka hupendelea
kuingia ndani ya eneo letu, lakini kwa sasa kwa sababu ya
doria tunazofanya mara kwa mara tatizo hilo limeweza
kudhibitiwa,”alisema.
Kwa upande wa ukataji wa miti, alisema walilazimika
kuelimisha jamii kuachana na ukataji wakuni na miti ya
kujengea nyumba zao, kwani eneo hilo ni kwa faida yao na
vizazi vyao vinavyokuja, baada ya kuona wanavyonufaika na
utalii sasa wao wamekua walinzi wakubwa.
Alisema watalii wanapokuja na kuhitaji ngoma za kitamaduni,
basi jamii ya kimasai inayonzunguka eneo hilo ndio inayotoa
burudani na kupata fedha
kwa ajili ya shughuli zao.
Nae afisa uhifadhi daraja la kwanza na afisa mawaliano ya
umma na masoko TAWA kanda ya Kaskazini Yuthnes Godfrey
Nestory, alisema eneo lao ni jipya na lina upekee na uzuri
ambao haupatikani kwenye hifadhi nyengine zozote
Tanzania.
Aliwataka wananchi kutumia nishati mbadala ya kupikia na
kuachana na matumizi ya kuni na mkaa, kufanya hivyo
wataweza kupunguza uharibifu wa mazingira kwa ukataji wa
miti, ikizingatiwa ndio kivutio cha
wanyamapori.
Hata hivyo nae Mkurugenzi wa JET JohN Chikomo,
alilishukuru shirika la USAID kupitia mradi wa Tuhifadhi
Maliasili unatekelezwa na JET, kwa kufanikisha ziara hiyo
kwa waandishi wa habari za Mazingira.
No comments:
Post a Comment