Na Fauzia Mussa Maelezo.05.05.2024.
Mkuu wa Oganaizesheni Afisi Kuu ya chama cha mapinduzi
Zanzibar Omar Ibrahim Kilupi amezitaka jumuiya za chama
cha Mapinduzi kuweka mikakati ya kuwatambua vijana ambao hawajasaliliwa katika datfari la wapiga kura ili waweze
kusajiliwa.
Akifungua kongamano la jumuiya ya wazazi wa Mkoa wa
Magharibi Kichama huko Skuli ya Ali Hassan Mwinyi Bububu
amesema kuna baadhi ya vijana hawakujiandikisha katika
awamu iliopita hivyo ni vyema kuwatambua na
kuwahamasisha kujiandikisha katika awamu ijayo.
Amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea vijana hao
kutojisajili kuwa ni pamoja na kutotimiza umri wa miaka 18
pamoja na kuwa mbali na vituo vya kujiandisha kwa kipindi
hicho.
Aidha amezitaka jumuiya hizo, kuhakikisha vijana wote
waliotimiza vigenzo wanajisajili ili kuweza kupata vijana
wengi watakaoendelea kukiweka madarakani chama cha
Mapinduzi ifikapo 2025.
“Kuna kundi la wananchi ambao wana sifa za kujisajili lakini
hawajaenda kujisajili na kama tunavyojuwa kama hukujisajili
katika daftari la kudumu la wapiga kura hutoweza kupiga
kura,tuendeni tukahamasishe ili tusije kumuacha mtu
nyuma.” alisema Kilupi.
Aidha amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya
uchaguzi na mmongonyoko wa maadili na kuwataka
kuyafanyia kazi mafunzo walipopewa sambamba na kuwa
mabalozi wazuri kwa wenzao.
Kwa upande wake Mlezi wa Mkoa wa magharibi kichama
ambae pia Mwakilishi wa viti maalum kupitia jumuiya ya
wazazi mkoa wa kusini Unguja Mhe. Sabiha Filfil Thani
amesema kuna kila sababu ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi
kuendelea kubaki madarakani katika Uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika hapo mwakani kutokana na kutekeleza kwa vitendo
ilani ya chama hicho.
“Ilani ya CCM ilimtaka rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi kujenga madarasa 1,500 kwa Skuli za
Unguja na Pemba ambapo amevunja rikodi kwa kujenga
madarasa 2273 sawa na silimia 150 ya malengo ya ilani ya
chama cha Mapinduzi.” amefahamisha Mlezi huyo.
Katika kongamano hilo mada mbili ziliwasilishwa na
kujadiliwa ikiwemo mmongonyoko wa maadili na uchaguzi
Mkuu ambapo Kauli mbiu ni ”USHINDI WA CCM 2024-
2025 JUMUIYA YA WAZAZI TUPO MSTARI WA MBELE”.
Vijana wa Sanaa wa kikundi cha Toto boy Hawai Ibrahim Juma Shaaban na Hamad Seif Mohammed wakitoa burudani yenye maadhui ya athari za mmong'nyoko wa maadili katika Kongamano la jumuiya ya wazazi, lililofanyika Skuli ya Ali Hassan Mwinyi Bububu Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAEEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment