Habari za Punde

Kocha Mkuu Timu ya Uhamiaji Abdi Saleh Ahaidi Ushindi Mchezo Wao wa Marudiano leo

Na.Mwajuma Juma.

KOCHA wa timu ya soka ya Uhamiaji Abdi Saleh, amesema hakuna sababu itakayowafanya washindwe kuwafunga wapinzani wao katika mchezo wao wa marudianao unaoschezwa leo nchini Libya.

 

Uhamiaji inashuka dimbani leo kucheza na Al-Ahly kucheza mchezo wao marudiano ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa nchini humo Uhamiaji ilifungwa mabao 2-0, hivyo ili kusonga mbele wanahitaji ushindi wa mabao 3-0.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Saleh alisema wachezaji wapo vizuri na wamejiandaa kushinda mchezo huo ambao ili kuweza kusonga mbele.

 

“Hakuna sababu ya kushindwa kuwafunga labda zitokee firigisu za waamuzi”, alisema kocha huyo.

 

Alieleza kuwa wachezaji wote wapo katika halinzuri ma mazingira waliyonayo ni mazuri sana na kila kitu kipo sawam hivyo wapo teyari kwa mchezo wao huo na wanakwenda kupindua meza.

 

“Al Ahly tushawaona na tumewajuwa uzuri wao na mapungufu yao, vijana wameongezeka ari pamoja na viongozi wana ari kubwa nikiamini tunaenda kuwaliza leo waarabu wa gadafi”, alisema.

 

Hivyo alisema kuwa wanamatajio makubwa ya kupita ikiwa waamuzi watatafsiri sheria vizuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.