Habari za Punde

DKT. NCHEMBA ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA JIJINI DODOMA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (kushoto), akizungumza jambo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ofisi ya Mhe. Waziri, Jijini  Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kikao kati yao kilichofanyika jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha -Dodoma)




Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.

Bi. Kwakwa alilakiwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.