Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Usiku wa Kuamkia Leo, Novemba 20, 2024, amepata fursa ya Kuonana na kubadilishana mawazo na Viongozi, pamoja na Watu Mashuhuri kutoka Taasisi na Mataifa mbali mbali, ambao ni Washiriki wa Mkutano wa Dunia kuhusu Utalii, Uchumi wa Buluu, Bahari na Mazingira, unaoanza leo Asubuhi, hapa Jijini Almeria, Nchini Hispania.
Kupitia Hafla hiyo Maalum, iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Jiji la Almeria kusini mwa Hispania, Mheshimiwa Othman, ambaye ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, pia amejumuika na Watu hao Mashuhuri, katika Chakula cha Usiku, kilichoandaliwa kwa Lengo la Kuwakutanisha na Kuwatambulisha baadhi ya Viongozi na Wakuu wa Misafara, kutoka Maeneo na Mataifa mbali mbali Duniani.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Kimataifa la 'Sun and Blue' linaloandaa Mkutano huo wa Kimataifa, imeongozwa na Meya ya Jiji la Almeria, Bi. Maria del Mar Vasquez Aguero.
Ndani ya Msafara wake katika Hafla hiyo, pia Mheshimiwa Othman wamembatana na Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa ambaye pia anasimamia Nchi ya Hispania, Balozi Ally Jabir Mwadin, pamoja na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Novemba 20, 2024.
No comments:
Post a Comment