Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wananchi katika Maziko ya Aliyekuwa Muanshi wa Habari wa ZBC Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Mhe. Khamis Yussuf Mussa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti ya kuusalia mwili wa Marehemu Biubwa Said Mbarak Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, aliyekuwa Muandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) iliyoongozwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume, iliyofanyika katika Msikiti Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024 na (kulia kwa Rais) Mume wa Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Khamis Yussuf Mussa na (kushoto kwa Rais) Baba mzazi wa marehemu Said Mbarak Suleiman.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Biubwa Said Mbarak aliyekuwa Muandishi wa Habari wa ZBC, ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Chum, baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti, iliyofanyika katika Msikiti wa Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024 na (kulia kwa Rais) Mume wa Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Khamis Yussuf Mussa na (kushoto kwa Rais) Baba mzazi wa marehemu Said Mbarak Suleiman.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Biubwa Said Mbarak aliyekuwa muandishi wa Habari wa ZBC, baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti iliyofanyika Msikiti Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024, na (kushoto kwa Rais) Baba mzazi wa marehemu Said Mbarak Suleiman
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Mume wa ya Marehemu Biubwa Said Mbarak aliyekuwa muandishi wa Habari wa ZBC, Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Khamis Yussuf Mussa,baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti iliyofanyika katika Msikiti Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, (ZBC) familia na waumini wengine wa dini ya Kiislam kwenye maziko ya aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Shirika hilo, marehemu, Biubwa Said Mbarak aliefariki dunia usiku wa kuamkia leo hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akitibiwa

Maziko hayo yamefanyika nyumbani kwao Marehemu Kwaalamsha, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi na baadae Al hajj Dk. Mwinyi alihudhuria sala ya maiti iliyohudhuriwa pia na wananchi mbalimbali.

Marehemu Biubwa kitaaluma alikua mwandishi wa habari, alipata mafunzo ya kada hiyo kwenye Chuo Cha Idara ya Habari Maelezo wakati huo mwaka 1999 na aliajiriwa na ZBC mwaka 2007, ambapo awali alikuwa mwandishi wa habari za mawio, kipindi maarufu kinachorishwa Kila siku asubuhi na ZBC, redio, akiwa miongoni mwa watangazaji wa mwanzo wa kipindi hicho tokea kilipoanzishwa mwaka 2000. 

Baadhi ya waandishi wa habari waandamizi, na wafanyakazi wa ZBC, wameelezea namna walivyomfahamu marehemu Biubwa katika kazi zao, kwamba alikua mchapakazi, mweledi na mwenye ushirikiano mzuri na wenziwe na kwamba ameacha pengo kwenye tasnia ya habari.

Marehemu Biubwa alizaliwa mwaka 1972 na amezikwa kijijini kwao Jumbi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amin.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.