Habari za Punde

Maofisa Mipango wa Wizara za Serikali Kuingiza Mafunzo ya Maradhi Yasioambukiza Katika Bajeti Zao Ili Wafanyakazi Waweze Kujua Vichocheo vya Maradhi Hayo.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar( Z-NCDA)  Dk. .Said Gharib Bilali akifungua Mafunzo Kwa Maafisa Mipango wa Wizara za Serikali katika Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto  Kidongo Chekundu,  Wilaya ya Mjini.

Baadhi ya Maafisa Mipango wa Wizara mbali mbali za Serikali akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar( Z-NCDA)  Dk. .Said Gharib Bilali 
katika Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto  Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini wakati wa Mafunzo Kwa Maafisa Mipango wa Wizara mbali mbali za Serikali.
Mkufunzi Omar Abdulla Ali akielezea kuhusiana na magonjwa ya NCDs, Kisukari na Shindikizo la damu  katika Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto  Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini  wakati wa mafunzo kwa Maafisa Mipango wa Wizara mbali mbali za Serikali.

Msaidizi Meneja Kitengo cha Maradhi yasioambukiza (NCDs  UNIT) Wizara ya Afya Zanzibar, Zuhura Saleh Amour akitoa mada kuhusiana aina ya Saratani katika Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto  Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini  wakati wa mafunzo kwa Maafisa Mipango wa Wizara mbali mbali za Serikali.

Na Khadija Khamis, WHVUM. 28/12/2024.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar( Z-NCDA)  Dk.Said Gharib Bilali amewataka Maofisa Mipango wa Wizara za Serikali kuingiza mafunzo ya maradhi yasioambukiza katika bajeti  zao ili  wafanyakazi waweze kujua  juu ya vichocheo vya maradhi hayo.

ameyasema hayo katika Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto  Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini wakati wa mafunzo kwa Maafisa Mipango wa Wizara mbali mbali za Serikali.

amesema ni vyema wafanyakazi wa serikali kupatiwa mafunzo ya Maradhi yasioambukiza  ili kuwa na taaluma sahihi ya visababishi vinavyochangia ongezeko la maradhi hayo pamoja na athari zake.

Aidha amesema maradhi hayo athari yake ni kubwa ambayo kuharibu muelekeo wa maisha kwa kupoteza uwezo wa kufikiri na kufanyakazi . 

amefahamisha kuwa maradhi yasioambukiza yako mengi lakini mengine ni hatari zaidi kutokana na gharama kubwa ya matibabu yake.

"Uhalisia wa  maradhi ya presha, sukari,  maradhi seli mundu (sickle cell ), Saratani na maradhi ya moyo, hayana dawa" amesema Mwenyekiti Dr. Said Gharib.

ameeleza kwamba Jamii ikipata muamko wa maradhi hayo itasaidia kupunguza ongezeko na kuleta mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha  ikiwemo kula mlo kamili wa matunda na mboga mboga pamoja na kufanya mazoezi ili kupunguza uzito mkubwa .

Kwa Upande wa Msaidizi Meneja Kitengo cha Maradhi yasioambukiza (NCDs  UNIT) Wizara ya Afya Zanzibar, Zuhura Saleh Amour amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la  maradhi yasioambukiza jambo ambalo linachangia kupoteza nguvu kazi ya taifa.

"Ni vyema sasa kila mtu ahakikishe analinda afya yake kutokana na vichocheo vya maradhi hayo."amesema Msaidizi huyo.

Amesema kwa kadiri umri unapozeeka ni hatari kupata maradhi hayo kutokana na kinga ya mwili kupungua uwezo wake wa  kufanyakazi ipasavyo.

kwa upande wa Muwasilishaji  mada katika mafunzo hayo Omar Abdulla Ali amesema changamoto zinazotokana na harakati za maisha huchangia, maradhi ya ugonjwa wa akili pamoja na shindikizo  la damu

Mada mbali mbali ziliwasilishwa ikiwemo ukubwa wa vichocheo vya maradhi yasioambukiza, Magonjwa ya NCDs Kisukari, Shindikizo la damu pamoja na Aina za Saratani .

mafunzo hayo ya siku mbili yametayarishwa na Jumuiya ya Muungano wa Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar  chini ya ufadhili wa (CISU) kupitia Jumuiya ya Cancer ya Denmark.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.