RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza
kwamba mambo yote anayoyatamka hadharani juu ya utekelezaji wa miradi mikubwa
zaidi ya maendeleo hapa nchini sio porojo za kisiasa bali ni dhamira yake ya
kweli ya utekelezaji.
Ameyasema hayo alipofungua maengesho ya
kwanza ya ghorofa Malindi Zanzibar, Shehiya ya Mchangani, Wilaya ya Mjini Mkoa
wa Mjini Magharibi ikiwa ni shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dk. Mwinyi amesema kufanya hivyo ni
kuonesha uongozi unaoacha alama na uzalendo pamoja na kuwahakikishia wananchi
kwa kauli mbio inayosema “yajayo ni makubwa zaidi.”
Akiitaja miradi mengine mikubwa ya
kimkakati inayotarajiwa kutekelewa miaka ijayo chini ya uongozi wake, Rais Dk.
Mwinyi amesema ni pamoja na mradi wa taxi za baharini ambapo ujenzi wa bandari
za taxi hizo umeanza Maruhudi zitakazo bakia na kushua abiria watakao tumia
usafiri wa maji kuelekea maeneo ya Mkoa wa Kaskazini unguja kwa kutumia taxi
hizo barala ya usafiri wa nchikavu wa daladala na usafiri mwengine, Mradi wa treni
zitakazotumia barabra za lami kutoka Malindi mjini hadi Bububu, ujenzi wa barabra
nne za juu zenye mapishano pamoja na ujenzi wa jeti kwa usafiri maji kwa ajili
ya kuwasafirishia watalii wanaotembelea visiwa vidogovidogo.
Katika hatua nyengine Rais Dk. Mwinyi amewatoa
hofu wananchi wa Mji Mkongwe kwamba Serikali inatekeleza miradi yake huku ikiwa
na dhamira njema ya kuuendeleza urithi wa Kimataifa ikiwa na lengo la kuulinda
mji huo na sio kuuharibu.
Amesema, uzinduzi wa maegesho ya magari
Malindi, una nia ya kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo
yanayoingia na kutoka Mji Mkongwe.
Pia Dk. Mwinyi amebainisha kuwa mbali na
maegesho hayo, ameeleza nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inakusudia
kujenga kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria, pembezoni mwa maegesho ya gari
Malindi, sabamba na ujenzi wa kituo kikubwa cha gari za abiria pamoja na
kiwanja cha michezo kwa vijana.
Amefahamisha kupitia mradi wa “Big Z”
Serikali pia inakusudia kujenga mradi wa barabara ya kisasa kutoka Malindi hadi
hospitali ya Mnazi Mmmoja ikiwa ni hatua ya kuupandisha hadhi Mji Mkongwe pamoja
na kuwa na mradi wa kuweka waya zote za umeme, maji na mawasiliano chini ya ardhi
ili kuimarisha usafi wa mji huo kwa kuikarabati umpya kwa kuiboreshea haiba
njema, bustani ya “Jamhuri garden” ili iwe na mwonekano wa kisasa.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameupongeza Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, ZSSF kwa kutekeleza wajibu wao wa kutoa mafao kwa
wananchi kwa wakati na kwa kiwango kizuri, kuwekeza kwenye miradi yenye tija na
kufanikiwa kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi kwa kujenga miradi mikubwa, akitolea
mfano mataifa mengine duniani kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ndio inayojenga
nchi, hivyo aliitaka ZSSF kuendeleza utaratibu huo.
Dk. Mwinyi pia amewasisitiza wanachi
kuendelea kuidumisha amani ya nchi, umoja na mshikamano ili nchi iendelee
kupiga hatua kubwa za maendeleo.
Amempongeza Mkandarasi wa Ujenzi huo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo KMKM na Mshauri elekezi kwa CCEC kwa
kufanikisha ujenzi wa maegesho ya gari, Malindi kwa viwango cha hali ya juu na
kuzingatia wakati.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mita na Idara Maalum za SMZ, Masoud
Ali Mohammed ambae pia amemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Saada
Mkuya Salum amesema, maendeleo anayoyaendeleza Rais Dk. Mwinyi amewafilisi watu
wasioitakia mema Zanzibar na wananchi watamkumbuka kwa kuacha alama ya uongozi
wake na kuonesha uzalendo alionao kwa nchi anayoiongoza.
Akibainisha gharama za ujenzi wa
maegesho hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Juma Malik
Akili amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 6.8 zilitumika kukamilisha ujenzi huo
wa kisasa na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuwasilisha michango yao ya ZSSF
ili miradi mikubwa zaidi ya maendeleo iendelee kutekelezwa na mfuko huo.
Ameleleza maegesho hayo yana uwezo wa kuchukua
gari 200 hadi 220 kwa wakati mmoja.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment