Habari za Punde

Tanzania na Czech Wajadili Kusaini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili

Mkuu wa Idara ya Uchumi na Biashara, Ubalozi wa Czech, Bi. Marta Anna Ledgard akizungumza katika kikao kati ya Tanzania na nchi hiyo kilichoongozwa na Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, kwa upande wa Tanzania na Balozi wa Czech Nairobi, Mhe. Nicol Adamcova’, jijini Dodoma. 

Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye na Balozi wa Czech Nairobi, Mhe. Nicol Adamcova’, wakiuongoza ujumbe wa Tanzania na Czech katika picha ya pamoja baada ya kufanya kikao kuhusu utiaji saini wa Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili kati ya nchi hizo mbili, ambao unatarajiwa kuweka mazingira ya kodi yanayotabirika ili kuvutia uwekezaji wa mitaji ya muda mrefu pamoja na kuondoa mzigo wa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji wanaondesha shughuli zao kati ya nchi hizo mbili, jijini Dodoma. 

Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, akiagana na Balozi wa Czech Nairobi, Mhe. Nicol Adamcova’, baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yao kuhusu utiaji saini wa Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili kati ya nchi hizo mbili, ambao unatarajiwa kuweka mazingira ya kodi yanayotabirika ili kuvutia uwekezaji wa mitaji ya muda mrefu pamoja na kuondoa mzigo wa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji wanaondesha shughuli zao kati ya nchi hizo mbili, jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

Na Farida Ramadhan,WF, DODOMA

Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu – El Maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Czech, uliongozwa na Balozi wa Czech nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcova, katika ofisi za Wizara ya Fedha, Jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, yalilenga utiaji saini wa Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech ambao unatarajiwa kuweka mazingira ya kodi yanayotabirika ili kuvutia uwekezaji wa mitaji ya muda mrefu pamoja na kuondoa mzigo wa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji wanaondesha shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.

Kikao hicho kilimshirikisha Kamisha Msaidizi wa Sera, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia masuala ya kodi za Kimataifa, Bw.Juma Mkabakuli.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech zilikamilisha majadiliano ya Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili mwaka 2024 na kwa sasa taratibu zote za kisheria za ndani kwa nchi zote mbili zimekamilika kwa ajili ya kusainiwa ili mkataba huo kuridhiwa na kuanza utekelezaji.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.